Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez amefanya ziara ya kutembelea mradi wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani kuangalia namna kiwanda hicho kinavyo ongeza thamani za zao la muhongo na kuboresha kipata cha wakulima.
Katika ziara hiyo, Bw. Alvaro Rodriguez aliongozana na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika ambaye shirika lake limekubali kusaidia kukiendeleza kiwanda hicho kupata mashine ya kisasa pamoja na uwezo wa nguvu kazi kuongeza ufanisi wa kiwanda.
Akizungumza katika kiwanda hicho, Bw. Malika alisema UNCDF imekubali kukisaidia kiwanda hicho ili kuinua hali ya kipato cha wakulima wa zao la muhogo wa Wilaya ya Rufiji ambao tayari walianza kuzalisha mazao hayo kwa kukitegemea kiwanda cha ‘African Starch Project’ ambacho kilisimamisha uzalishaji kutokana na uwezo mdogo wa mashine zake. “…UNCDF tumekubali kutoa mtaji wa kuanzia pamoja na kuwezesha nguvu kazi ili kiwanda kiweze kujiendesha kibiashara na kuendelea kuwanufaisha wakulima wa zao la muhogo eneo hili…tayari wamehamasika na kilimo hiki baada ya kuletwa kwa mradi huu sasa tunataka kuuongezea nguvu zaidi,” alisema Kiongozi na Mshauri wa Ufundi wa Shirika la UNCDF, Malika.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (kushoto) wakiangalia sehemu ya tawi la mmea wa muhogo uliopo shambani walipotembelea moja ya mashamba ya wakulima wa mihogo Wilaya ya Rufiji jana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape waendeshaji wa mradi huo alisema kwa sasa wakulima zaidi ya 500 wa zao la muhogo wameanza kunufaika na mradi huo ambao wamekuwa wakitegemea kukiuzia kiwanda muhogo wa kuchakata jambo ambalo limekuza kipato chao.
Alisema ufadhili wa UNCDF utakapokamilika kimtaji katika kiwanda chao zaidi ya wakulima 7000 watakuwa wakinufaika ndani ya miaka miwili, ambapo zao wanalolilima litaitajika kwa wingi kiwandani hivyo kuboresha hali za kiuchumi kwa jamii, lakini lengo kwa hapo baadaye ni kuhakikisha wakulima 10000 wananufaika na shughuli nzima za mradi huo wa kiwanda.
Aliongeza kuwa kwa sasa zaidi ya vijiji 20 wilayani Rufiji vinavyozunguka kiwanda hiko wananchi wake wapo tayari kufanya biashara ya kilimo kukipatia kiwanda muhogo wa kuchakata, ambapo watakuwa wakishiriki kuwawezesha wananchi katika vikundi ili waweze kufanya uzalishaji wa kutosha kiwandani.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez(kushoto) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana. Kulia ni Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika.
Kwa upande wao baadhi ya wakulima wakiwemo akinamama waliozungumza katika ziara hiyo wamelishukuru shirika la UNCDF kwa kufadhili kiwanda hicho kwani tendo hilo limewahakikishia upatikanaji wa soko la uhakika kwa zao la muhogo, ambalo hapo awali lilikuwa likilegalega kutokana na kupoteza kiasi kikubwa cha mabaki ya zao hilo.
UNCDF inategemea kutumia takribani shilingi milioni 400 kwa ajili ya kukiwezesha kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo eneo hilo.
Ziara ya viongozi hao ambao waliambatana na wajumbe wa manamawasiliano wa mashirika ya umoja wa mataifa iliwafikisha katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji na kufanya mazungumzo na viongozi wa halmashauri kujua changamoto anuai za kijamii.
Mtaalamu wa Mawasiliano, Ushirikiano na Utafutaji Mitaji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Jacqueline Namfua akiwatambulisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika (katikati) kwenye ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji walipotembelea ofisi hizo jana.
Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezo.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) akipata maelezo eneo ambalo mtambo unaosha muhogo kabla ya kuanza uchakataji. Katikati ni Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape akitoa maelezo.
Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania ukiongozwa naMratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez ukitembelea maeneo mbalimbali ya kiwanda.
Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (kushoto) akielezea namna kiwanda hicho kinavyofanya kazi. Kutoka kulia wanaomsikiliza ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja, Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez.
Ujumbe huo ukipata maelezo sehemu ya mitambo ya kiwanda cha kuchakata zao la muhogo inavyofanya kazi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim Hape (aliyenyoosha mkono).
Mkurugenzi Mtendaji Kanda wa FJS African Starch Development, Ibrahim M. Hape (wa kwanza kushoto) akiwaelezea wajumbe waliotembelea kiwanda hicho namna kinavyofanya kazi. Ujumbe huo wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania uliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (wa tatu kulia). Kutoka kulia ni Ofisa Habari wa Shirika la Kazi Duniani nchini Tanzania, Magnus Minja na Peter Malika Kiongozi wa UNCDF.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.
Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akizungumza na baadhi ya wakulima wanaonufaika na kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu, Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani jana walipofanya ziara katika mradi huo uliombioni kusaidiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF) kwa manufaa ya wakulima wa muhogo eneo hilo.
Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na baadhi ya wanahabari na ujumbe wa wanamawasiliano (hawapo pichani) baada ya ziara ya kukitembelea kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo eneo la Bungu Wilaya ya Rufiji jana.
Mmoja wa wakulima wa muhogo wanaonufaika na uwepo wa kiwanda cha kuchakata zao la muhogo ‘African Starch Project’ kilichopo Kata ya Bungu akielezea wanavyonufaika kwa ujumbe wa wanamawasiliano wa mashirika ya UN nchini Tanzania walipotembelea mradi huo jana Wilaya ya Rufiji Mkowa wa Pwani.
Kutoka kushoto ni Mtaalamu wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Hoyce Temu, Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Kiongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Mitaji (UNCDF), Peter Malika wakitembelea moja ya mashamba ya zao la muhogo wilayani Rufiji jana.
from Blogger http://ift.tt/1TTNFv9
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment