Simba mmoja Nairobi, Kenya amemjeruhi mtu mmoja nchini humo baada ya Simba huyo kufanikiwa kutoka katika moja ya hifadhi zilizopo katika mji mkuu huo wa Kenya.
Mfanyakazi mmoja wa kituo cha huduma kwa wanayama nchini humo, Paul Udoto amesema Simba huyo alifanikiwa kumjeruhi mtu huyo ambaye ana miaka 63 ambapo alipelekwa hospitali ili kupata huduma.
Pia Udoto amesema bado wanaendelea na kufanya juhudi ili kumrudisha Simba katika hifadhi hiyo na hali ya mtu aliyejeruhiwa inaendelea vizuri hospitalini ambapo alipelekwa kupata huduma.
from Blogger http://ift.tt/1TTNFv2
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment