UVCCM NJOMBE WAOMBA RAISI KUKAZA UZI

RAIS wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Dr. John Magufuli ameombwa kuendelea na kasi hiyo ili kuwa wasaidia watu wa hali ya chini waliokuwa wakinyanyasika kutokana na vitendo vya ufisadi vilivyokuwa ukiendelea hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuwafirisi wale wanao bainika kutafuna pesa za wananchi.
Ombi hilo limetolewa na umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi UVCCM mkoa wa Njombe baada ya kuona kasi anayoendanayo inaenda kuboresha maisha ya watanzania kwa kubana mianya ya rushwa na kutolewa kwa elimu bure.
Wakizungumza katika mkutano wa tathimini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana vijana wa umoja huo walisema kuwa wanamuomba Rais kuhakikisha kuwa anakaza uzi na kasi aliyoanzanayo ili kuimarisha uchumi wa nchi.
Vijana hao  walisema kuwa kile anacho kifanya Rais ni kuweka sawa masuala ya uchumi kuwapandisha wasio nacho na kukaribia wale walio nacho na kuw ana uchumi wa kati.
Sylvester Mgimba mkazi wa Ludewa alisema kuwa vijana wote Tanzania waungane na Rais kupambana na Ufisadi wa mali za umma na kuwasaidia walio kuwa wananyonywa na kumuunga mkono juhudi zake za kukusanya kodi.
Alisema kuwa kukiwapo na Rais wa aina hiyo kunakuwa na watua wanao mpingia wanaopinga ni moja kati ya watu ambao walikuwa na maslahi katika ubadhilifu.
“Nchi ilikokuwa inaenda ilikuwa inapotea sasa tumepata mkombozi wa watanzania na amekuwa kuinyoosha Tanzania katika njia sahihi maana nchi iliko kuwa inaenda ilikuwa inapotea” alisema Happy Mpete mkazi wa Makambako.
Alisema ukamuaji wa majipu anao ufanya Rais Magufuri watu wasichukie maana wananzania wa hali ya chini wamenyanyashwa vya kutosha na kuwa kutokana na ukamuaji huu watanania tunaelekea kwenye neema.
Mwenyekiti wa Uvccm mkoa, Iman Fute alisema kuwa mabadiliko anayo yafanya Rais nndio yalikuwa yanahitajika na watanzania wengi kwa kuwa vitendo vilivyo kuwa vinatpokea havikuwa vinakemewa sasa mkemeaji amepatikana na nchi inakuwa katika msitali na watumishi kuwatumikia wananchi sawasawa.
Alisema kuwa kama vijana wanampongea Rais kwa kuanzisha huduma ya elimu bure kwa watanzania na kuwa mpango huo umeongeza watoto wa kitanzania kuingia shuleni.
“Sasa inaonyesha ni jinsi gani watanzania walikuwa hawapati elimu kutokana na gharama za ada shuleni sasa vijana wengi wanakwenda shule kwaajili ya kupata elimu kwa hili tunapongeza sana kasi ya Rais Magufuli,” alisema Fute.
Aidha katibu wa CCM Hosea Mpagike aliwataka vijana hao kuhakikisha kuwa wanamsaidia Rais katika kasi yake na kufichua wale wanao fanya ubadhilifu mdogomdogo huko vijijini kwas kuwa nchi hii ni kubwa hivyo wawafichue.
Mpagike alisema kuwa vijana wahakikishe kuwa taarifa wanazo zitoa za majipu madogo madogo kuwa yanatumbuliwa kwa kutolewa  taafira za uhakika ili kuokoa pesa za miradi mbalimbali.
“Vijana toeni taarifa za kuwapo kwa ubadhirifu huko vijijini kwa kuwa nchi hii ni kubwa Rais hawezi kufika kila kona tumsaidie kuibua wabadhilifu katika kila kona za nchi yetu ili kuhakikisha kuwa miradi inasimamiwa ipasavyo,” alisema Mpagike.

from Blogger http://ift.tt/1UNeTyE
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment