WAKAZI jijiji cha Utweve kata ya Ukwama wilayani Makete mbele ya mkuu wa wilaya hiyo Veronica Kessi wanaapa kuto endelea na shughuli za maendeleo kutokana na watuhumiwa wa mauaji ya mtoto Fedy Sanga (17) May 31 kurejea kijijini kwao na kutamba.
Marehemu kabla ya kifo chake alituhumiwa na wanafamilia hao kuwa ni mwizi kitu kilicho wafanya wakazi hao kutokubaliana nacho kwa kuwa wanafahamu mtuhumiwa wa wizi hapashwi kuuwawa badala yake alipaswa kupelekwa polisi.
Katika mkutano wa kwanza wa mkuu wa wilaya ya Makete kukutana na wananchi anakutana na makubwa ambapo wananchi wanamueleza kelo yao na kumtaka ashughulikie watuhumia wanao tamba mtaani sheria itende haki na wao kuanza kufanya maendeleo.
Mama wa mtoto aliye uwawa alisema kuwa baada ya watuhumiw akurejea kijijiji hapo alitambiwa kuwa zinafungwa pesa na kuwa hawataweza kufungwa masikini ndio wanafungwa.
Atu Sanga ni mama wa marehemu aliangua kilio mbele ya mkuu wa wilaya kutokana na kauli alizo kuwa akizisikia kutoka kwa watuhumiwa na kuwa ni siku chache tangu kuzikw akwa mwanae.
Wananchi hao wakiwa na uchungu wa mtoto wa kijijini kwao kudaiwa kuuwawa na watuhumiwa watatu wanafamilia na kukaa ndani kwa wiki mbili na kurejea kijijini hapo wanataapa kuto fanya shughuli za maendele.
Abraham Tete alisema kuwa kijijini hapo hawata fanya maendeleo mpaka ufafanuzi wa watuhumiwa hao kupatikana kijijini hapo na kuwa ujenzi wa Zahanatu sasa umesimama kutokana na tatizo hilo.
Alisema kuwa mkutano wa mapato na matumizi uliokuwa ufanyike kijijini hapo ulivurugika kwa kuwa ufafanuzi wa jamo hilo ulikuwa haujapatikana kijijini hapo.
Mwanasheria wa halmashauri Godfrey Masunga baada ya kuwasikia wananchi anawataka waache mahakama ifanye kazi yake na kuwa wananchi hao wabadilishe mtazamo na kuelekea katika shuguli zao za kimaendeleo za kila siku.
“Kisheria polisi ndio wanafanya uchunguzi wa kesi na kupeleka maelezo mahakamani na anaye amua kesi hii iwe ya aina gani ni askali kulingana na upelelezi alio ufanya” alisema Masunga.
Hata hivyo mkurugenzi wa halmashauri ya makete Francis Namaumbo anawataka wananchi hao kuendele na shughuli za kimaendeleo na kuwaomba suala hilo waiachie mahakama ifanye kazi yake.
Baada ya kusikia kero hizo kutoka kwa wananchi mkuu wa wilaya Kesi anawaomba wananchi hao kuendelea na shughuli za kimaendeleo kijijini hapo na kuwa suala lao linashugulikiwa.
Aidha mwenyekiti wa kijiji hicho Rauteli Sanga alisem akuwa sasa suala lao litashughulikia na kuwaomba atakapo waita katika shughuli za maendeleo kuhakikisha kuwa wanajitokeza na kuendelea kukiletea maendeleo kijiji chao na kuwa kijiji cha mfano kwa wilaya ya makeni.
from Blogger http://ift.tt/29Xy0ak
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment