KAMPENI YA USAFI WA MAZINGIRA YAINGIA AWAMU YA PILI

MKAZI WA KIJIJI CHA WELELA 
Mwenyekiti wa kijiji cha Welela Danny Ngimbhudzi
Wataalamu kutoka wizara ya afya na halmashauri wakifanya ukaguzi wa vyoo bora
Mathias Gambishi afisa afya mkoa wa Njombe
MKAZI WA KIJIJI CHA WELELA AKITOKA SAMBA NA NDOO YA MAJI KICHWANI
MOJA YA VYOO BORA KULIKO MAKAZI KATIKA KIJIJI CHA WELELA CHOO CHA MZEE

IMEDAIWA kuwa kuwapo kwa kampeni ya usafi wa mazingira katika vijiji vya halmashauri ya wilaya ya Njombe magonjwa ya kuhara yamepungu hasa kwa watoto wa shule za msingi huku asilimia kubwa ya kaya zikiwa na vyoo bora vya masinki na kutumia maji.
Hayo yanabainishwa na Mwalimu mkuu wa shule ya msingi WelelaMwl. Gabriel Mdenye ambayo inatekeleza kampeni hiyo licha ya kuwapo kwa shida ya kuyapata maji shuleni na katika jamii ya wakazi wa baadhi ya vijiji vya halmashauri hiyo.
Alisema kuwa vyoo bora vya kutumia masinki vimeanza kutumika katika shule yake na magonjwa ya kuhala kwa wanafunzi wake yamemalizika hii inaonyesha mafanikio katika zoezi lao la kampeni ya usafi wa mazingira.
Alisema kuwa pamoja na kuwapo kwa vyoo hivyo safi lakini kila asubuhi sharti wanafunzi waanze na kuchota maji katika kisima kilichopo shuleni hapo na kujaza katika matanki ya maji karibu na vyoo kwaajili ya usafi wa vyoo na wanafunzi wenyewe kunawa mikono.
Nao baadhi ya wakazi wanasema kuwa wamekuwa wakifanya usafi wa vyoo vya kwa shida kwa kuwa vyoo hivyo bila maji ni sawa na hakuna na kuwa kijijini hapo hakuna maji na huwalazimu kutembea kwa zaidi ya kilomita moja kufuata maji ambayo ni ya kisima.
Anna Gadao anasema kuwa pamoja na kuwapo kwa kampeni hiyo wanaomba serikali kampeni hiyo kuendana na kuleta maji karibu na makazi yao ili kuepukana na adha hiyo ya maji.
Aidha katika kijiji hicho mwenyekiti wake Danny Ngimbhudzi  anasema kuwa wamekuwa wakiilizwa mara kwa mara kuhusiana na upatikanaji wa maji hasa pale wanapo wahimiza ujenzi wa vyoo hivyo vinavyo hitaji maji.
Hata hivyo baadhi yao wanapongeza juhudi za serikali kuwaletea utaratibu huo ambapo Agness Motto anasema kuwa baada ya kuanzishwa kwa kampeni hiyo hawaugua magonjwa ya kuhara.
Kampeni hiyo mwaka huu imeingia katika awamu ya pili ikiwa sasa inalenga kubadili maisha ya watanzania kuingia katika hali ya usafi ikiwa ni lengo la kiulimwengu kufikia mwaka 2030 kila mwanadamu kuwa na choo bora lakini kwa hapa nchini ni kufikia hatua ya juu mwaka 2025.
Afisa afya mkoa wa Njombe Mathias Gambishi,  anasema kuwa awamu ya kwanza imekamilika mwaka huu mwezi Juni na kuwa  awamu ya pili imeanza mwaka huu ambapo kwa mwaka huu kwa vijiji ambavyo vilifanya kampeni hiyo vitakuwa katika ugaguzi na tathimini ya matumizi ya vyoo.
Aidha wataalamu kutoka wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia watoto na wazee na maafisa afya wanaingia katika ukaguzi wa ujenzi wa vyoo bora, ambapo vyoo sasa ni bora kuliko majengo ya kuishi vinyesi vichakani hakuna.
Anyitike Mwakitalima mratibu wa chanjo na usafi wa mazingira, anasema kuwa katika ukaguzi wao wanabaini kuwa kila kaya ina choo bora cha sinki huku ukaguzi huo pia ukilenga sehemu ya kunawia mikono, kichanja cha kuanzikia vyombo na shimo kwaajili ya kuterketezea taka.

from Blogger http://ift.tt/2dR4U2Q
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment