|
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho Mashaka Gambo,
amewasimamisha kazi watumishi watatu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro kwa
tuhuma za ubadhilifu wa fedha za uchaguzi wa mwaka 2015.
Na Mwandishi wetu,
Watumishi hao ni pamoja na Bi. Hadija Mkumbwa ambae
alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kumfuta cheo hicho,bwana Evansi Mwalukasa alikuwa
mwekahazina wa halmashauri na bwana Sembeli
Sinayo yeye alikuwa mwanasheria wa halmashauri.
Maamuzi hayo yamefikia baada yakubainika kuna
upotevu wa fedha za uchagu takribani Milioni
188 ambazo matumizi yake hayakuwekwa
wazi na pia Milioni 20 zilitumika kwa manunuzi ambayo hayakufuata
taratibu za manunuzi ya serikali.
“Kuanzi sasa nawasimamisha kazi hawa watumishi watatu kwasababu
wameisababishia serikali hasara ya takribani Milioni 128 ambazo zilikuwa fedha
za uchaguzi”.
Aidha Muheshimiwa Gambo alisema maamuzi hayo
yametokana na taarifa aliyokabidhiwa na kamati aliyoiunda yakuchunguza mapato
na matumizi ya fedha za halmashauri hiyo na kubaini upotevu huo wa fedha nyingi
ambazo zingeweza kusaidia shughuli mbalimbali za uchaguzi katika Wilaya hiyo.
Ambapo fedha nyingine zimetumika kwenye manunuzi
ambayo hayakufuata taratibu na sheria za manunuzi ya serikali ,hivyo ni kinyume
kabisa na taratibu za serikali katika maswala ya manunuzi.
Akisisitiza kwa watumishi wa serikali kufuata
taratibu, sheria na kanuni mbalimbali katika kutekeleza majukumu yao ili
kuepuka migongano na uvunjifu wa sheria mahala pa kazi nakupelekea kupoteza
kazi zao.
|
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Ngorongoro wakimsikiliza Mkuu wa
Mkoa (hayupo pichani),alipokuwa akizungumza nao baada yakufanya ziara
katika ofisi za halmashauri hiyo, Wilayani Ngorongoro.
from Blogger http://ift.tt/2dJ2DBL
via IFTTT
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment