Bombardier 3 mpya za Air Tanzania mbioni kutua nchini


 

Kampuni ya ndege ya Bombardier inatarajia kuzileta ndege tatu mpya kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL, imefahamika.
cwynnlrucaacozw
Ndege hizi mbili ni aina ya CS300 na moja ya Q400. Ndege hizo zina thamani ya dola milioni 203.
Mwishoni mwa Septemba mwaka huu, Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt John Magufuli aliahidi kununuliwa kwa ndege zingine mbili kubwa kwaajili ya shirika la ndege la Tanzania, ATCL.
Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa ndege mbili mpya za kwanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.

Ndege hizo ni aina ya Bombadier Q 400 zilizotengenezwa nchini Canada.
Alisema ndege mbili kubwa zitakazonunulia hapo baadaye zitakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine kubwa zaidi itakayobeba abiria 240 pamoja na mizigo yao. Aliwahakikishia Watanzania kuwa fedha za kununua ndege hizo zipo.

Ndege za sasa zina uwezo wa kubeba abiria abiria 76, 6 wakiwa daraja la juu na 70 ni daraja la chini
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment