
Kampuni
ya simu ya Tecno hii leo December 3 2016 imezindua kampeni ya Christmas
ambayo inawawezesha wateja wake kujishindia tiketi za safari ya kuzuru
nchini Uingereza katika kampeni inayokwenda kwa jina la #KamaMbele.
Uzinduzi huu ni katika jitihada za Tecno kuwapatia wateja wake zawadi
katika msimu huu wa sikukuu za Christmas na mwaka Mpya na kuwawezesha
kununua simu bora kwa gharama nafuu hivyo kuwawezesha kufurahia pamoja.
Katika
kampeni hii mwanadada mrembo anayeng’arisha video za mastaa wa Bongo
(Video Vixen), Hamisa Mobetto na mshindi wa Big Brother Africa –
Hotshots mwaka 2014, Idris Sultan ni mabalozi wa kampeni hii ambapo
mmoja wao kati ya Idris au Hamisa atashinda safari ya Uingereza
akiambatana na shabiki mmoja.
Hivyo ili mteja uweze kushiriki shindano hili unatakiwa kuingia kwenye tovuti ya shindano ambayo ni http://tecnokamambele.co.tz/,
utapiga kura kwa supar staa mmoja kati ya Idris au Hamisa kisha
utaeleza kwanini unaikubali Tecno yako ukitumia hashtag #KamaMbele na
shabiki mshindi atapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na mashabiki
katika hatua ya pili ya shindano.
Mbali na
kujishindia safari ya kwenda nchini Uingereza, wateja wa Tecno na
Watanzania kwa ujumla wataweza kujishindia zawadi mbalimbali na kupata
punguzo la bei katika simu za Tecno. Unaweza kutazama video hii kwa
kuingia http://tecnokamambele.co.tz/, na kumpigia kura Idris Sultan uwe kwenye nafasi ya kuibuka mshindi wa Safari.
0 maoni:
Post a Comment