
Leo
December 03 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli, amefanya uteuzi wa Mabalozi 15 ili kujaza nafasi zilizo wazi
katika Balozi za Tanzania zilizopo katika nchi mbalimbali. Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa
Mabalozi hao wameteuliwa kwa ajili ya kuiwakilisha Tanzania katika vituo
vifuatavyo;
⦁ Beijing – China
⦁ Paris – Ufaransa
⦁ Brussels – Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
⦁ Muscat – Oman
⦁ Rome – Italy
⦁ New Delhi – India
⦁ Pretoria – Afrika ya Kusini
⦁ Nairobi – Kenya
⦁ Brasilia – Brazil
⦁ Maputo – Msumbiji
⦁ Kinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
⦁ Kampala – Uganda
⦁ Abuja – Nigeria
⦁ Moroni – Comoro
⦁ Geneva – Umoja wa Mataifa
⦁ Beijing – China
⦁ Paris – Ufaransa
⦁ Brussels – Makao Makuu ya Jumuiya ya Nchi za Ulaya
⦁ Muscat – Oman
⦁ Rome – Italy
⦁ New Delhi – India
⦁ Pretoria – Afrika ya Kusini
⦁ Nairobi – Kenya
⦁ Brasilia – Brazil
⦁ Maputo – Msumbiji
⦁ Kinshasa – Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
⦁ Kampala – Uganda
⦁ Abuja – Nigeria
⦁ Moroni – Comoro
⦁ Geneva – Umoja wa Mataifa
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi wa Mabalozi 6 kwa ajili ya
kuiwakilisha Tanzania katika Balozi mpya 6 ambazo zitafunguliwa hivi
karibuni katika nchi za Algeria, Israel, Korea ya Kusini, Sudan, Qatar
na Uturuki.
Orodha kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni kama ifuatavyo;
⦁ Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
⦁ Balozi Samuel W. Shelukindo
⦁ Balozi Joseph E. Sokoine
⦁ Balozi Silima K. Haji
⦁ Balozi Abdallah Kilima
⦁ Balozi Baraka Luvanda
⦁ Balozi Dkt. James Alex Msekela
⦁ Bw. Sylvester Mwakinyuke Ambokile
⦁ Pindi Chana
⦁ Dkt. Emmanuel J. Nchimbi
⦁ Rajab Omari Luhwavi
⦁ Lut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace Mella
⦁ Grace Mgovano
⦁ Mohamed Said Bakari
⦁ Job Masima
⦁ Omar Yusuf Mzee
⦁ Matilda S. Masuka
⦁ Fatma M. Rajab
⦁ Sylvester M. Mabumba
⦁ Prof. Elizabeth Kiondo
⦁ George Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)
⦁ Balozi Mbelwa Brighton Kairuki
⦁ Balozi Samuel W. Shelukindo
⦁ Balozi Joseph E. Sokoine
⦁ Balozi Silima K. Haji
⦁ Balozi Abdallah Kilima
⦁ Balozi Baraka Luvanda
⦁ Balozi Dkt. James Alex Msekela
⦁ Bw. Sylvester Mwakinyuke Ambokile
⦁ Pindi Chana
⦁ Dkt. Emmanuel J. Nchimbi
⦁ Rajab Omari Luhwavi
⦁ Lut. Jenerali (Mstaafu) Paul Ignace Mella
⦁ Grace Mgovano
⦁ Mohamed Said Bakari
⦁ Job Masima
⦁ Omar Yusuf Mzee
⦁ Matilda S. Masuka
⦁ Fatma M. Rajab
⦁ Sylvester M. Mabumba
⦁ Prof. Elizabeth Kiondo
⦁ George Madafa (Uteuzi wake ulishatangazwa)
Vituo vya
kazi vya mabalozi hawa 21 vitatangazwa baadaye. Mabalozi wote waliobaki
katika vituo ambavyo si kati ya vituo hivi 15 vilivyotajwa wataendelea
na nafasi zao za uwakilishi wa Tanzania katika vituo walivyopo.
Katika
hatua nyingine, Rais Magufuli amemhamisha Balozi Modest Jonathan Mero
kutoka kituo chake cha sasa cha Geneva, kwenda Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa (New York) ambako atakuwa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania
katika Umoja wa Mataifa.
Balozi
Modest Jonathan Mero anachukua nafasi ya Mhe. Balozi Tuvako M. Manongi
ambaye atastaafu ifikapo tarehe 06 Desemba, 2016. Katika hatua nyingine,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Bibi Grace A. Martin kuwa Balozi na
Mkurugenzi wa Itifaki (Chief of Protocal) – Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki kuanzia leo tarehe 03 Desemba, 2016.
Kabla ya
uteuzi huo Grace A. Martin alikuwa akikaimu nafasi hiyo. Wakati huo huo,
Rais Magufuli amemteua Balozi Peter Kallaghe kuwa Afisa Mwandamizi
Mwelekezi – Mambo ya Nje katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National
Defence College) Kabla ya uteuzi huo, Balozi Peter Kallaghe alikuwa
Balozi wa Tanzania nchini Uingereza hadi mwanzoni mwa mwaka huu 2016.
0 maoni:
Post a Comment