Mchezaji wa klabu ya Manchester
City ambaye yupo kwa mkopo katika klabu ya Stoke City, Wilfried Bony
amejipanga kumfungulia mashitaka wakala wake wa zamani pamoja na klabu
ya Swansea City katika jitihada za kurejesha kiasi cha paundi milioni
8 ambayo anaamini ni mapato yake aliyoingizwa mjini na kuyapoteza.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28,
akikipiga kwa mkopo katika klabu ya Stoke City, amemfungulia mashitaka
wakala wake wa zamani ambaye pia alikuwa mwakilishi wake, Francis Kacou
kuhusiana na fedha zilizochukuliwa pasipo ruhusa yake katika usajili
ulimhusu yeye akitokea klabu ya Vitesse Arnhem kwenda Swansea mwaka 2013
na baadae alipoelekea katika klabu ya Manchester City mwaka 2015. Bony
pia anaishutumu klabu ya Swansea kuwa ilikuwa inafahamu mchezo mzima.
Malalamiko ya awali yalifunguliwa katika
jiji la Manchester siku ya Jumanne wiki hii lakini kusikilizwa kwa
mashitaka hayo kumehairishwa kutokana na kusubiriwa kwa maamuzi ya wapi
kesi hiyo inatakiwa kusikilizwa. Kacou, pamoja na mfanyabiashara
mwenzie Dalibor Lacina, pia wameomba muda ili waweze kukusanya taarifa
sahihi na ushahidi kwa utetezi wao.
Lakini kama inavyoweza kuwa bahati mbaya,
Kacou atakuwa anagombea nafasi katika mkutano mkuu wa Nchi ya f Ivory
Coast National Assembly siku ya Jumapili, December 18 ambayo kama
atashinda inaweza kumpa kinga ya kisiasa kwa maana ya kukwepa kesi yake
kusikilizwa nchini Uingereza.
Kacou pia amekuwa katika mgogoro na winga
na mchezaji wa Bournemouth Max Gradel na beki wa zamani wa vilabu vya
Arsenal na Sunderland, Emmanuel Eboue ambaye anatumikia kifungo cha
mwaka mmoja kujihusisha na soka kutokana na kushindwa kumlipa wakala
wake.
Swansea walilipa kiasi cha paundi milioni
12 (£12million) kwa Vitesse kumsajili Bony na baadae akajiunga na
Manchester City kwa kiwango kinachokadiriwa kuzidi paundi milioni 25
(£25m).
Bony yupo katika mkopo katika klabu ya
Stoke City yenye maskani yake kwenye uwanja wa Britannia lakini ana
kipengele kwenye mkataba wake kinachomruhusu kuuzwa kwa klabu ya China
mwezi Januari kama atahitajika.
Msemaji wa Swansea City alisema: ‘Hili ni jambo linalomhusu Bony pamoja na wawakilishi wake, sie hatumo.’
‘Bahati mbaya tumeingizwa kwenye matatizo
yake kwa sababu tu tulihusika katika kuuzwa kwake mara zote mbili, mara
ya kwanza ikiwa kumleta hapa na nyingine ikiwa kumuuza kwenda Manchester
City.’

0 maoni:
Post a Comment