Gerlad Chesoli: Muziki wa Injili wa Kenya Umepoteza Mwelekeo..


Mwimbaji wa Nyimbo Injili nchini Kenya Gerlad Chesoli amedai kuwa muziki wa Injili nchini humo umepoteza mwelekeo kwa kiasi kikubwa.
Akiongea na ripota wa GospoMedia nchini Kenya Gerlad amedai waimbaji wengi wa Injili nchini Kenya wametoka kwenye maudhui makuu ya muziki huu ambao ni kuhubiri injili na kuufanya kuwa wakiburudani zaidi.
Gerlad ametoa wito kwa vyombo vya habari vya nchini humo kucheza nyimbo za Injili za kweli .
Fuatilia mahojiano yote ya Gerlad Chesoli na GospoMedia.

jichopembuzi: kwa kifupi jitambulishe kwa wafuatiliaji wa GospoMedia.. Gerlad: Nafahamikakama Gerald chesoli ,mimi ni msaani wa injili ,mzaliwa wa mji wa kitale. jichopembuzi: Ni lini na nini kilicho kuchochea kuanza kuimba nyimbo za injili? Gerlad: Nilianza kuimba mwaka wa 2006,kama mmoja wa waimbaji wa kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu kanisani kwetu.nilichochewa na roho mtakatifu kuanza kuhudumu kama mwimbaji binafsi na hapo nikaona makuu na miujiza ya Mungu. jichopembuzi: Tangu umeanza kuimbaumejifunza nini na imekusaidiaje kama mwimbaji? Gerlad: Nimejifunza kuwa na subira na pia upendo kwa wale wote nafanya nao kazi haya yote yamenifanya kupata wakati wa kuendelea kuwa kama mwimbaji .
Gerlad: Ni changamoto zipi kama msaani unakumbana nayo katika huduma yako? Gerlad: Changamoto ni nazo zipitia ni kama za kifedha na pia kupata mahali pakuperform kama mwana mziki.
jichopembuzi: Una mtazamo gani juu ya Muziki wa Kenya?
Gerlad: Muziki wa kenya haswa wetu wa kiinjili umepoteza maudhui makuu ambayo ni kuendeleza injili ,na amini kwa kuabudu kwa ukweli na ndiposa ni maombi yangu kuwa mungu atainua watu wamuabudu kwa roho na kweli .
jichopembuzi: kwa kuwapa wasomaji wetu ufahamu wa mziki wako tutajie baadhi ya nyimbo zako Gerlad: Baadhi ya nyimbo zangu ni baraka,mpenzi yesu,rehema ,mimi sonko ,usiniache,neema,moving and ushukuriwe.
jichopembuzi: Unawezaje kuandika nyimbo zako mwenyewe? Gerlad:Roho Mtakatifu ananichochea zaidi katika uandishi wa nyimbo zangu.
jichopembuzi: Ni nani haswa unamuangalia kama role model wako? Gerlad: Kirk Franklin kwa sababu ni mwimbaji wa kuabudu na pia wakati wake wakuabudu yeye huabudu bila kuwa na uigizaji .
jichopembuzi: Kama ungepewa fursa ya kubadili kitu kwenye muziki wa Injili,je ungebadili nini ? Gerlad: kwanza ningezungumza na wanahabari wazidi kucheza nyimbo za injili za kweli

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment