Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, George Kyando amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Inadaiwa kuwa, Miseyeke alifanya kitendo hicho juzi saa tano asubuhi katika pori lililopo katika kijiji cha Kipeta, katika Bonde la Ziwa Rukwa, wilayani Sumbawanga.
Akisimulia mkasa huo Kamanda Kyando amesema, siku ya tukio Chela ambaye ni mkazi wa kijiji cha Legezamwendo kilichopo katika Bonde la Ziwa Rukwa wilayani Sumbawanga aliingia ndani ya pori hilo la akiba bila ya kibali.
“Chanzo cha tukio hilo ni baada ya kijana Salaganda Chela kukaidi amri halali ya kusimama na kukamatwa. Mbinu iliyotumika ni kumpiga risasi mguu wa kushoto baada ya kumtahadharisha kwa ofisa wa wanyapori kupiga risasi kumi hewani," amesema Kamanda Kyando.
Amesema, mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi kwa mahojiano zaidi kwa kuwa alitumia nguvu nyingi kupita kiasi na kwamba, Chela hakuwa na hakuwa na silaha.
Chela amelazwa wodi namba 3 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa, mjini Sumbawanga.
Anasema, siku hiyo ya tukio alipigwa risasi na ofisa wa wanyamapori akiwa nje ya pori la akiba la Uwanda.
“Nilikuwa niko karibu na pori la akiba la Uwanda ghafla nikawaona askari wa wanyapori nikaogopa kwani wana tabia ya kukamata watu kisha kuwalazimisha kuingia ndani ya pori hilo la akiba kisha wanawaadhibu kwa madai kuwa wameingia bila vibali. Nilianza kukimbia huku askari watatu wa wanyamapori wakinifukuza hadi nikachoka , nikaingia ndani ya nyumba kwa ajili ya usalama wangu ndipo mmoja wao akinifyatulia risasi za moto huku tukio hilo likishuhudiwa na wanawake na watoto , risasi hizo zilinijeruhi vibaya na kuuvunja mguu wangu wa kushoto," amedai.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Rukwa , Dk John Lawi amesema, majeruhi huyo alipokelewa hospitalini hapo juzi saa 12 jioni hali yake ikiwa mbaya.
Wadogo wa majeruhi Kidoga Chela (26) na Singu Chela (28) wamesema, kwa nyakati tofauti kuwa kaka yao alipigwa risasi huku wanawake na watoto waliokuwa kwenye nyumba aliyokimbilia kujificha wakishuhudia.
Singu amesema, "Askari wa wanyamapori walimkamata wakamfunga pingu kisha wakamwingiza kwenye gari lao na kumkimbiza katika kituo cha afya kilichopo kijijini Kipeta ambapo alipatiwa huduma ya kwanza.
Amesema, baada ya kupatiwa huduma ya kwanza askari hao wa walitumia gari kumpeleka kituo cha polisi kama mtuhumiwa akiwa na pingu mikononi.
"Ndipo walipoona hali yake inazidi kuwa mbaya askari wa kituo cha polisi kilichopo katika wilaya ya kipolisi Laela walikubali tumuwekee dhamana ya maneno kisha akaletwa na kulazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa matibabu,” amesema Singu.
0 maoni:
Post a Comment