Mbunge wa jimbo la Mikumi na msanii wa muziki wa Bongo fleva Prof Jay ameitumia vyema siku ya kuuaga mwaka 2016 kwa kumvisha pete ya uchumba mzazi mwenzake Grace Mgonjo zikiwa ni harakati za kuelekea kufunga ndoa.
Prof Jay akimvisha pete ya uchumba Grace Mgonjo
Prof Jay mwaka jana kupitia kipindi cha Planet bongo aliahidi na kusema kuwa haitapita muda mrefu sana watu wataanza kupewa kadi kwa ajili ya ndoa yake na sasa hizi ni dalili kuwa huenda ndoa hiyo ipo siku za karibuni.
"Asante sana Mungu, leo (Jana) tunaufunga mwaka namna hii na Mke wa Profjize" aliandika Prof Jay katika picha akiwa anamvisha pete ya uchumba Grace Mgonjo