Umeme hakuna kupanda- Rais Magufuli




Zikiwa zimepita siku mbili toka Mamlaka ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeridhia ombi la Shirika la umeme nchini TANESCO la kupandishwa kwa bei ya umeme kwa asilimia 8.5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Rais John Pombe Magufuli
Mh. John Pombe Magufuli ameungana na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kupinga hatua iliyochukuliwa na EWURA.

Rais Magufuli akiwa mjini Bukoba leo amesema suala la kupandishwa bei ya umeme lilikuwa ni suala la mtu mmoja kulingana na nafasi yake na kwa kitendo hicho Rais anakiri kuwa bado kwenye Serikali kuna majipu meni na ataendelea kuyatumbua.

"Namshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini ameshatengua maamuzi ya EWURA kwa hiyo umeme hakuna kupanda, haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati hii mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpka vijijini, na umeme huu unaenda mpka wa watu masikini walioubwa kwa mfano wa Mungu harafu mtu pekee kwa sababu ya cheo chako unakwenda unasimama na kwenda kupandisha bei ya umeme. Na ndiyo maana baba Askofu nalizungumza hili kwamba majipu bado yapo mengi na nitaendelea kuyatumbua " alisema Rais Magufuli 

Mbali na hilo Rais Magufuli amewaomba Watanzania waendelee kuwaombea kwani lengo la serikali anayoiongoza ni kwenda na wananchi wa chini 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment