Akatwa Mkono Baada ya Kufumaniwa na Mke wa Mtu

POLISI katika Kaunti ya Kisii nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo mwanamume mwenye umri wa miaka 40 alikatwa mkono katika kijiji cha Matongo, Kaunti ya Kisii kwa madai ya kula uroda na mke wa mtu.
Bw Richard Omoke aliyejeruhiwa, alipatikana akiwa amelala na mke wa mwanamume aliyemkata jikoni mwa mwanamke huyo. Mumewe mwanamke huyo alimshambulia kwa kutumia upanga na kuukata mkono wake hadi ukaanguka kando.
Mume huyo, Bw Vincent Gwaro mwenye wa miaka 35, alienda kuwaita majirani washuhudie kisa hicho nyumbani kwake lakini akatoroka, na polisi walikuwa wanaendelea kumtafuta.
Mke wake pia alitoroka baada ya kisa hicho.
Chifu wa eneo hilo Bw John Motobwa alisema Bw Gwaro aliwaambia wakazi kuwa bibi yake alikuwa anashiriki ngono na mwanamume mwingine jikoni mwa nyumba yake.
“Alimuumiza vibaya huyo mzee na kumwachia majeraha mabaya mwilini,” alisema Bw Motobwa.
Bw Chrisantus Asanyo ambaye ni mkazi wa eneo hilo alisema Bw Gwaro alikuwa amewaita kwake ili kushuhudia kisa hicho.
Walipofika katika nyumba hiyo ndipo walipompata Bw Omoke akiwa na maumivu makali, hajitambui, huku akilitamka jina la Vincent.
“Aliacha mkono ukiwa umekatwa na hapakuwa na dalili ya kuonekana kwa bibi yake hapo karibu. Bw Gwaro alitoroka baadaye,” alisema Bw Asanyo.
Aliongeza kuwa wawili hao walikuwa marafiki wa karibu sana na walikuwa wakifanya biashara pamoja. 
Akithibitisha kisa hicho, Mkuu wa Polisi katika eneo la Marani Bw Benjamin Kimwele alisema kisa hicho kilitendeka mwendo wa saa tatu usiku wa kuamkia jana.
Aidha, Bw Kimwele aliongeza kuwa polisi wameanzisha uchunguzi kuhusiana na kisa hicho na wanaendelea kuwasaka hao wawili ili kuandikisha taarifa.
Aliyejeruhiwa alipelekwa katika Hospitali ya Kimisheni ya Tenwek kwa matibabu zaidi.
“Mwathiriwa alikuwa na majeraha manne kwa kwa kichwa chake, shingo na mgongo,” alisema.
Mkuu huyo wa polisi aliwaonya wananchi dhidi ya kuchukua sheria kwa mikononi mwao, bali wawe wakipiga ripoti kwa polisi.
“Msichukue sheria mikononi mwenu wakati mizozo ya kinyumbani inapozuka. Muwaache polisi wafanye kazi yao ya kutatua uhalifu,” akasema Bw Kimwele.

from Blogger http://ift.tt/2kVtyOK
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment