BOSI WA GOOGLE AJIBU BARUA YA MTOTO WA MIAKA SABA ALIYEOMBA KUFANYAKAZI KWENYE KAMPUNI HIYO

Kuna watoto wanaopenda kuja kuwa wana anga, zima moto au wapishi watakapokuwa wakubwa – lakini mtoto mmoja nchini Uingereza ameelekeza akili yake yote kwenye moja ya kampuni bora kabisa za teknolojia duniani kwa sasa.
Mtoto huyu, Chloe Bridgewater, ana umri wa miaka 7, aliandika barua na kuituma kwenye kampuni ya Google akielezea uwezo wake wa kutumia kompyuta na kueleza pia nia yake ya kuja kufanya kazi kwenye kampuni hiyo yenye viti vya Maputo (ambavyo hujazwa upepo) na magari madogo ambayo wafanyakazi wanaendesha wakiwa wanatoka sehemu moja ya ofisi kwenda nyingine wawapo kazini.
Chloe (7) alituma barua hii aliyoiandika kwa mkono kwenda kwa Mkurugenzi wa Google
‘Bosi wa Google’, Mkurugenzi Mtendaji Sundar Pichai, alimjibu mtoto Chloe kwamba ‘anasubiri kupokea’ barua yake ya maombi ya kazi na kumsisitiza afuate ndoto zake mpaka zitapotimia.
Chloe anayeishi mji wa Hereford aliamua kuandika barua hiyo baada ya kuona picha ya ofisi za kampuni ya Google zikiwa zimejaa viti vya kujaza upepo na magari hayo.
Magari yaliyopo ndani ya majengo ya Google ambayo wafanyakazi wanayatumia kutoka ofisi moja kwenda nyingine
Katika barua aliyoiandika. Chloe alimwambia Bwana Pichai, ambaye kwenye barua hiyo amemuita jina la ‘Bosi wa Google’, kwamba anapenda kutumia kompyuta na kucheza ‘game’ kutumia tablet yake ambayo huutumia kumuongoza roboti.
Pia aliandika kuwa baba yake amemwambia kwamba akiendelea kuwa mwanafunzi mzuri kama alivyo sasa na akawa anafaulu shuleni, ipo siku atapata kazi kwenye kampuni ya Google – Chloe aliongeza kuwa anataka afanye kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza ‘chocolate’ na vilevile anapenda kuja kuwa muogelea kwenye mashindano ya kimataifa ya Olimpiki.
Familia ya bwana Bridgewater ikapokea barua ya majibu kutoka kwa Mkurugenzi huyo mwanzoni mwa mwezi huu akimpa moyo mtoto Chloe na kumwambia aendelee kufanyia akazi ndoto zake mpaka zitakapotimia.
Barua ambayo Mkurugenzi Mtendaji wa Google aliiandika kujibu barua ya mtoto Chloe
‘Nafurahi kwakuwa unapenda kompyuta na roboti, nategemea utaendelea kujifunza mengi yanayohusu teknolijia,’ ameandika bosi huyo.
‘Bila shaka ukiendelea kufanya kazi kwa bidii na kufata ndoto zako, utatimiza kila kitu utakachoamua kufanya – kufanya kazi hapa Google na kuogelea katika mashindano ya Olimpiki.
”Nasubiri kupokea barua yako ya maombi ya kazi utapomaliza masomo yako’.
Sundar Pichai, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Google
Andy Bridgewater aliweka kwenye akaunti yake ya LinkedIn barua hiyo aliyojibiwa na bosi wa Google. Alieleza kuwa binti yake huyo alipata ajali ya gari miaka michache iliyopita, na kwamba barua hiyo kutoka Google imemfariji sana binti yake.
‘Baada ya kupata ajali ya gari miaka kadhaa iliyopita, alikuwa hajiamini tena,’ aliandika kwenye akaunti yake ya LinkedIn.
‘Hata hivyo, nikisema kuwa Cloe alifurahi alipopata barua hii iliyotoka kwa bwana Sundar Pichai mwenyewe itakuwa sijaelezea vizuri hisia zake.’
‘Sasa anaonekana kuwa na hamu zaidi ya kuhakikisha anafaulu shuleni ili akafanye kazi kwenye kampuni ya Google.’
Wafanyakazi wa Google wakiwa wamekalia viti vya kujaza upepo
‘Nashindwa kutoa shukrani zinazostahili kwa bwana Pichai ambaye yupo bize sana lakini akatenga muda wake kufanya binti wangu asogee hatua moja mbele kuitimiza ndoto yake, ingawa sina hakika kama anajua kwamba kuweza kufanya kazi Google ni zaidi ya kukaa kwenye viti vya kujazwa upepo na kuendesha magari ndani ya ofisi!’
Mtoto Chloe Bridgewater aliandika kwamba baba yake, Andrew alimwambia kama ataendelea kuwa mwanafunzi mzuri na kufaulu atafanya kazi Google

from Blogger http://ift.tt/2kG1iP3
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment