Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema wanachama na viongozi wake 125 wamefunguliwa kesi katika Mahakama mbalimbali nchini tangu kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
CHADEMA imesema wanachama hao wamepandishwa kizimbani katika jumla ya kesi 78 huku wengi wao wakinyimwa dhamana na wale na wale waliopatikana na hatia walipewa adhabu za vifungo bila ya kupewa fursa ya faini.
Kutokana na hali hiyo, CHADEMA inatarajia kuandaa orodha itakayoainisha kesi zote za jinai ambazo bado zipo Mahakamani pamoja na kuonesha aina ya mashtaka na vifungo vilivyotolewa, kwa vyombo vya habari na taasisi za ndani na nje ya nchi.
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Profesa Abdallah Safari aliyasema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mrejesho wa kikao cha kamati ndogo ya Kamati Kuu ya CHADEMA kilichokaa Jumanne. Profesa Safari alisema kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu kumalizika, viongozi wa CHADEMA wamekuwa wakikamatwa na kushtakiwa kwa makosa ya kubambikizwa, kwa kisingizio cha uchochezi.
“Hivi sasa umekuwa ni mtindo wa Mahakama kuwakatalia dhamana wanachama wa CHADEMA bila ya sababu za msingi. Pia imekuwa ni mtindo kuwahukumu vifungo bila kuwapa fursa ya kulipa faini. Majaji wanapaswa kuiga mfano wa uhuru wa Mahakama na weledi wa majaji wa Afrika Kusini, Zimbabwe na Marekani ambao waliweza kutengua amri batili zilizotolewa na marais wa nchi zao,” alisema Profesa Safari.
HT: NIPASHE
MAADILI YAPOROMOKA MASHULENI WANAFUNZI WASHINDANA KUCHEZA NA KUONYESHA NGUO ZA NDANI
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
from Blogger http://ift.tt/2m2JY7Q
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment