Eric Omondi: Namshukuru Sana Diamond, Ndiye Aliyenifungulia Mlango Kwenye Soko la Tanzania

Mchekeshaji maarufu kutoka nchini Kenya, Erick Omondi ijumaa iliyopita ya tarehe 10 alifunguka jinsi Diamond alivyomsaidia kupenya kwenye soko la Tanzania.
Omondi anasema kwa mara ya kwanza alikutana na Diamond Mombasa nchini Kenya akiwa kwenye harakati za kurekodi wimbo wa Diamond unaoitwa Nabeba Mawe.
Katika mazungumzo yao Diamond alimualika Omondi kwenye show kubwa maarufu kama “Zari All White Part” na kumuomba awe MC wa show.
Katika show hiyo ambayo ilikuwa na zaidi ya wahudhuriaji 10,000 , redio na TV nyingi za Tanzania Omondi hakufanya kosa kama MC, alitumia kudhihirisha kipaji chake cha uchekeshaji na ikawa ndio mwanzo wa kujulikana Tanzania.
Omondi anasema bila Diamond kumwalika Tanzania huenda asingeweza kupenya katika soko la Tanzania, soko lenye mashabiki wengi sana wa kazi zake.
Mpaka sasa Erick Omondi ana mpango katika kipindi cha miezi miwili ijayo, kuanzisha Comedy TV show nchini Tanzania kwenye moja ya Runinga maarufu hapa nchini.
Japo hakuweka wazi kipindi hicho kitarushwa hewani kupitia kituo cha habari cha shirika lipi.
Source: NTV ya nchini Kenya.

from Blogger http://ift.tt/2kZnuXG
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment