Wakati makampuni mengi yakijiondoa kufanya kazi na binti mkubwa wa Rais Donald Trump wa Marekani, Ivanka, bintiye mwingine, Tiffany anakumbana na mikausho pia.
Tiffany alijikuta akitengwa na watu kwenye siti ya mbele aliyokuwa amekaa kushuhudia show kwenye New York Fashion Week. Mtoto huyo wa Trump alikuwa amewekewa kiti cha mbele kabisa lakini akajikuta akikaa mwenyewe baada ya watu kumkimbia.
Mwandishi wa masuala ya fashion, Christina Binkley alitumia Twitter kueleza kuwa hakuna aliyetaka kukaa karibu na binti wa rais huyo mtata. Amedai kuwa wahariri wawili wa mambo ya fashion, walibadilisha viti kuepuka kukaa karibu na binti huyo mwenye miaka 23.
“Nobody wants to sit next to Tiffany Trump at Philipp Plein, so they moved and the seats by her are empty,” aliandika Christina Binkley.
Pia alipost picha ya viti vitupu karibu na Tiffany Trump.
Muigizaji mkongwe na mtangazaji wa kipindi cha The View, Whoopi Goldberg amemtetea Tiffany kwenye video hiyo chini.
from Blogger http://ift.tt/2m1bNO8
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment