Mbunge wa zamani Kinondoni, Iddi Azzan amezungumzia sakata lake na Jeshi la Polisi baada ya kukaa mahabusu kwa siku mbili alikokuwa akihojiwa kuhusu kuhusishwa kwake na masuala ya dawa za kulevya.
Mapema jana akiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Azzan alisema aliingia katika orodha ya watuhumiwa kwa kuwa amekuwa akisemwa katika mitandao ya kijamii kwa muda mrefu.
Hata hivyo, alisema alifurahishwa na kitendo cha kutajwa kwenye orodha ya wanaojihusisha na biashara hiyo akiamini kwamba hatimaye suala hilo litafikia mwisho.
“Bora nilivyotajwa huenda suala hili litaisha kwa kuwa nimeanza kusemwa tangu mwaka 2011. Cha ajabu ni kwamba awali nilituhumiwa kujihusisha na biashara sasa hivi napimwa kuona kama natumia.
Mbunge huyo pamoja na Askofu Josephat Gwajima walitoka polisi saa 10:28 baada ya kuitukia wito uliowataka kuripoti hapo jana saa nane mchana.
Wakati Azzan aliondoka kituoni hapo kwa gari aina ya Toyota Rav 4 ‘short chassis’, Askofu Gwajima aliondoka kwa teksi.
from Blogger http://ift.tt/2lis4AY
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment