Lissu ni Shiidaaha.. Amnyoosha Kamanda wa Polisi Mahakamani..!!!

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kamanda wa polisi wa Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani wamechuana mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili mbunge huyo na wahariri wa gazeti la Mawio.
Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba leo atatoa uamuzi wa kama Hamdani aeleze anachokifahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
Hiyo ilikuwa ni baada ya Lissu kumtaka Hamdani, ambaye ni shahidi wa upande wa mashtaka, aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar na kama Jecha anaweza kufuta matokeo ya uchaguzi.
Hakimu Simba alifikia uamuzi huo baada ya wakili wa Serikali, Paul Kadushi kupinga shahidi huyo kujibu swali hilo kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala katiba hivyo hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.
Lissu alimhoji Hamdani maelezo yake yaliyo polisi aliyaandika kama nani? Mahojiano yao yalikuwa kama ifuatavyo:
Hamdani: Niliandika maelezo yangu kama mlalamikaji na kwamba mikusanyiko hiyo haikuwa haramu, ilikuwa halali kisheria.
Lissu: Mweleze mheshimiwa kama mihemko kisheria inakatazwa ama la?
Hamdani: Haikatazwi.

from Blogger http://ift.tt/2kIPi09
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment