Imevuja..Kipigo Chamtoa Mbio Gigy Money kwa Mwanaume Huyu..!!!

UHUSIANO wa kimapenzi uliotawaliwa na sarakasi nyingi, kati ya muuza nyago machachari Bongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ na mtangazaji mwenzake wa kituo kimoja cha redio nchini, Moulad Alpha ‘Moj’ hatimaye umevunjika baada ya mwanadada huyo kusalenda kutokana na madai kwamba mchizi alikuwa akimshushia sana kichapo mwanadada huyo.
Kwa mujibu wa chanzo chetu kilichopo karibu na wawili hao, licha ya Gigy kuonekana machachari kwenye jamii, tangu aanzane na Moj aliamua kutulia mno, tatizo ni kwamba jamaa hajatulia na kila anapomuhoji kwa nini anamsaliti anampa mkong’oto.
“Habari ndo hiyo, wale wameshaachana maana mara kwa mara Gigy alikuwa anapigwa kwa kosa ambalo si lake, amevumilia sasa uzalendo umemshinda,” alisema sosi.
Kwa upande wake Gigy alipotafutwa, alisema alikuwa anampenda sana Moj kwani alimuona ni mstaarabu lakini ghafla amebadilika sana.
“Kweli kupenda utumwa, mateso niliyoyapata kwa huyu mwanaume nimesalenda, kwa nini haniheshimu na ananipiga?” alisema Gigy

from Blogger http://ift.tt/2lm6LPn
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment