Sekeseke la Madawa Masogange Kufikishwa Kortini Kesho…!!!

KAMANDA wa Polisi wa Kanda Maalumu Dar es Salaam, Simon Sirro amesema mtuhumiwa, Agnes Gerald maarufu Masogange na wenzake 15 wamepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kuchukuliwa vipimo vya damu ili kubaini kama wanatumia dawa za kulevya.
Staa huyo wa video za wasanii wa Bongo Fleva anayetajwa kama ni miongoni mwa mastaa wanaochukua fedha nyingi kama ujira wa kucheza katika nyimbo mbalimbali za wasanii kama video queen, anahushishwa na madawa ya kulevya kwa mambo matatu ambayo atachukuliwa vipimo. ni pamoja na kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya.
Masogange alikamatwa na polisi juzi na alifikishwa kituoni kwa mtindo tofauti na wasanii wengine kwani yeye hakutangazwa kama ilivyokuwa kwa Wema, T.I.D, Nyandu Tozi na wengine wakiwemo wafanyabaishara wakubwa Dar es Salaam.
Kamishna Sirro amewaambia wanahabari leo kuwa Masogange amepelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali na majibu yakipatikana kesho atafikishwa mahakamani kama itakuwa itakuwa ni tofauti anaweza kufikishwa kortini jumatatu.
“Tunamchunguza Masogange katika mambo matatu ili kujua kama anauza , anatumia au anasafirisha dawa za kulevya, “ amesema Kamishna Sirro.

from Blogger http://ift.tt/2kui5Jy
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment