Je, kompyuta yako ipo slow? Fahamu njia saba za kuifanya kompyuta yako kuwa na kasi tena



Katika vitu vinavyokera zaidi kama wewe ni mtumiaji wa kompyuta ni kitendo cha PC yako kuwa slow. Kuna sababu nyingi zinasababisha kompyuta kuwa slow kama virusi, hardware specification pamoja na RAM kuzidiwa mzigo.


Matumizi ya kompyuta hotofautiana sana kutoka mtumiaji mmoja mpaka mwingine kulingana na aina na shughuli inayofanyiwa. Kompyuta kwa matumizi ya kuchapa, kusikiliza muziki pamoja na kuangalizia muvi huwa hazihitaji hardware specifications kubwa ukilinganisha na kompyuta za kufanyia graphics na kuchezea games.

Mara nyingi watumiaji wengi wa kompyuta hulalamika kuwa kompyuta zao zimekuwa slow sana tofauti na hapo awali wakati wanazinunua. Kuna sababu nyingi zinazofanya kompyuta kuwa slow kama nilivyoeleza hapo juu inategemea sana na matumizi ya kompyuta husika.
Njia 7 za kuifuata kama kompyuta yako ipo slow sana

1. Weka Anti Virus

Moja ya sababu kubwa ya kompyuta kuwa slow ni uwepo wa virusi vya kompyuta. Virusi vya kompyuta vitatumia sehemu kubwa ya RAM na HDD katika kutekeleza majukumu yake. Hivyo ni muhimu kuweka anti virusi nzuri na nyepesi ambayo haitatumia kiasi kikubwa cha RAM.

2. Futa Temporary Files

Kwa watumiaji wa Windows unaweza ukafungua my computer=>Nenda local disk C: au disk yenye Windows=> Fungua Users => Chagua User kama jina la mtumiaji lipo => AppData=> Local=>Temp

Hapo unaweza ukafuta mafaili yote yaliyomo kwenye hilo folder la temp, kisha restart kompyuta yako.

3. Punguza vitu katika Hard Drive yako

Kujaa kwa Hard drive kunachangia sana kompyuta kuwa slow. Windows inatoa taarifa ya kukaribia kujaa kwa hard drive yako mapema sana pale tu inapokaribia kujaa na kuibadilisha rangi na kuwa nyekundu. Futa au hamisha baadhi ya vitu ili kuiacha kompyuta yako ikiwa na nafasi ya kutosha.

4. RAM ya kompyuta yako ni ndogo, ongeza RAM

RAM ni kiungo cha muhimu sana linapokuja suala la speed (kasi) ya kompyuta husika. Kiasi cha RAM hotofautiana kulingana na bei ya kompyuta. Angalia mwongozo wa RAM kulingana na mfumo endeshi wa kompyuta yako;
Windows XP kiasi kidogo cha RAM kiwe 1GB
Windows 7 kiasi kidogo cha RAM kiwe 2GB
Windows 8, 8.1 na 10 kiasi kidogo cha RAM kiwe 4GB

Ukiachana na RAM bado kuna vitu vingi vya kuzingatia hapa kama processor, unaweza ukasoma zaidi hapa.

5. Funga baadhi ya Programs kama unarun Programs nyingi kwa pamoja

Kama umefungua programu nyingi kwa pamoja katika kompyuta yako ni vyema ukafunga baadhi ya programu ili kuipunguzia mzigo kompyuta.

6. Update Windows yako (Mfumo endeshi)

Ni muhimu sana kuupdate windows yako kila updates zinapotoka sababu updates zinakuja na maboresho mengi hasa ya kuisalama katika kompyuta yako.

7. Punguza Add-Ons kwenye browser (kivinjari) yako

Wingi wa Add-on kam vile youtube downloader, ruler, games, znet hupunguza ufanisi wa kompyuta kwa kiasi kikubwa sana, hivyo hakikisha unaunistall baadhi ya add-on ambazo huzitumii mara kwa mara.

Ni muhimu sana kununua kompyuta inayoendana na shughuli zako ili kuepusha uzumbufu usio wa lazima.

from Blogger http://ift.tt/2ksVYmM
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment