SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inakusudia kutunga sheria ya kuzuia uvutaji wa sigara hadharani katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Hatua hiyo ilitangazwa jana na Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo, wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Mpendae kwenye Baraza la Wawakilishi.
Mwakilishi huyo, Mohammed Said Dimwa, alitaka kujua athari kubwa inayopatikana kutokana na utumiaji wa sigara pamoja na mikakati ya wizara katika kukabiliana na hali hiyo.
Waziri huyo alisema serikali imeamua kuchukua hatua hiyo kutokana na uwapo wa idadi kubwa ya wagonjwa wa maradhi yasiyoambukiza na kwamba uvutaji wa sigara umebainika kuwa chanzo chake.
Kombo alisema katika kukabiliana na hali hiyo, Serikali itatenga maeneo maalum ya uvutaji wa sigara.
from Blogger http://ift.tt/2kZrIPm
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment