LIVE: Kamishna Madawa ya Kulevya Azungumza na Wanahabari, Ataja Mambo Mazito

Kamishna wa Operesheni ya Kupambana na Madawa ya Kulevya, Mihayo Msikela amezungumza na wanahabri leo Makao Makuu ya Mamlaka hiyo, Upanga Dar es Salaam.
Akizungumza na wanahabari Mihayo amesema;
“Vita hii haijaanza leo, ilianza mwaka 1995 zikatungwa sheria na mwaka 2016 ikaundwa tume maalum ya kupambana na madawa.
Kama dunia inapigana hivi vita na sisi lazima tupigane mpaka kutokomeza biashra hii haramu”. Alisema Kamishna Mihayo.
Kuhusu Mateja kufiikishwa mahakamani, Kamanda Mihayo anasemaje?
“Siyo Yusuf Manji pekee ndiye kafikishwa mahakamani, mateja wengi tu wengi wameshafikishwa mahakamani na wanashughulikiwa.” Alisema Kamishna Mihayo.
Kuhusu Sober House?
“Walioko kwenye Sober Houses, kwa mujibu wa uanzishwaji, Sober sio kwamba ni sehemu ya utumiaji wa madawa ya kulevya, na ikibainika watu wanafanya hivyo tutawashughulikia…
“Tunataka walioko sober wapone, waruudi wajumuike na Watanzania wenzao katika ujenzi wa Taifa. Alisema Kamishna Mihayo.
Kuhusu Oparesheni ya Kupambana na Madawa ya Kulevya yanayoingizwa nchini kutokea nchi za jirani.
“Mapaka sasa Mkoa wa Lindi ndiyo unaongoza, tumefanikiwa kukamata gramu 50 za madawa ya kulevya aina ya heroine kwenye mkoa huo, ikifuatiwa na mka wa Songwe na mikoa mingine inafanya juhudi… Vita hii ni ya wote, tuungane kupambana na kutokomeza bishara haramu ya madawa ya kulevya.” Alimaliza Kamishna Mihayo.

from Blogger http://ift.tt/2lqgm7X
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment