Mfanyaabiasshara alala mbele na EFd’s za wenzake

SERIKALI imetoa amri ya kusakwa na kukamatwa mfanyabiashara na wakala mmoja wa usambazaji wa mashine za kielekroniki (EFD) ambaye anadaiwa kukusanya fedha za wafanyabiashara wenzake na kutokomea nazo tangu mwaka 2013 bila ya kuwapa mashine hizo.
Amri ya kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Mecki Sadiki, baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wanaodai kutapeliwa.
Mkuu huyo wa mkoa alipata malalamiko hayo juzi wakati akizungumza na wafanyabiashara 180 wa maeneo mbalimbali ya mkoa huo kwa ajili ya kujadili changamoto zinazowakabili na kutafuta ufumbuzi wake pamoja na kujenga mazingira rafiki ya kufanyia kazi zao.
“RPC (kamanda wa polisi wa mkoa) mtafuteni mahali popote alipo wakala huyo ambaye amepewa jukumu la kusambaza mashine za risiti za kielektroniki. Mfanyabiashara huyu anadaiwa alichukua fedha za wafanyabiashara wenzake bila kuwapa mashine hizo tangu mwaka 2013 hadi sasa.”
“Kitendo hicho ni sawa na wizi na hakiwezi kuvumiliwa na serikali kwa kuwa kinasababisha Mamlaka ya Mapato (TRA) kukosa mapato kutoka kwa wafanyabiashara ambao walikuwa na nia ya kulipa mapato,” alisema Sadiki.
Kwa upande wake, Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Philip Kimune, alisema ofisi yake imepokea orodha ya wafanyabiashara 48 wanaowalalamikia mawakala kutowapa mashine hizo licha ya kuzinunua kwa gharama kubwa.
Naye Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Kilimanjaro, Hillary Lyatuu, alisema serikali inapaswa kusikiliza kilio chao na kuwasaidia kupata mashine hizo.

from Blogger http://ift.tt/2l0x9xa
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment