MAKONDA UWAFIKIE VIGOGO WA UNGA

Jumla ya watu 35 ambao ni polisi 17 pamoja na 18 ambao ni wasanii na watu wengine wametajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhamis ya wiki hii wakituhumiwa kujihusisha kwa namna moja ama nyingine na madawa ya kulevya (matatumizi au usambazaji wake)
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mh. Paul Makonda
Mkuu wa Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu, tayari amewasimamisha kazi polisi 12 kati ta 17 waliopo kwenye orodha hiyo ili kupisha uchunguzi unaolenga kubaini sababu za wao kuhusishwa na swala hili.
Mkuu wa Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu
Lengo la uchunguzi huu ni kwamba taarifa zitazopatikana zisaidie mamlaka kujua majina ya wauzaji au wafanyabishara wanaoshirikiana na watuhumiwa, taarifa ambazo zitasaidia mamlaka kwenda kwenye kiini cha tatizo hili.
Kwakuwa zimekuwepo taarifa mitaani zikiwataja hata baadhi ya viongozi wa serikali na wabunge kuwepo kwenye mtandao wa biashara ya dawa za kulevya nchini, bado taarifa hizo zitabaki kuwa tetesi tu kwakuwa majina hayo hayajatolewa au kuthibitishwa na mamlaka husika. Endapo mahojiano ya watu hawa wa sasa yataleta uthibitisho juu ya wale waliokuwa wakinyooshewa vidole kwa miaka mingi sasa, basi yawezekana ikawa hatua kubwa sana kuwahi kufikiwa katika nchi hii kwenye swala la kupambana na madawa haya yanayopoteza nguvu kazi ya Taifa letu.

from Blogger http://ift.tt/2kuGyLu
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment