MBUNGE RIDHIWANI KIKWETE AZUNGUMZIA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mkoani Pwani Ridhiwani Kikwete, amezungumzia kuhusu sakata la dawa za kulevya na kuipongeza serikali hususani Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaa, Paul Makonda kwa kuanzisha vita hiyo na kutaka wahusika wachukuliwe hatua.
Mbunge huyo ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mrisho Jakaya Kiwete ameyasema hayo leo katika kipindi cha Radio cha East Africa.
Aidha, ametumia nafasi hiyo kuishauri Serikali kuifikisha mwisho vita hiyo, ili kulimaliza kabisa tatizo hilo kwa kuwa limepoteza vijana wengi wenye uwezo mkubwa na mchango katika taifa, huku akitolea mfano uwezo wa msanii wa Bongo Fleva, Langa ambaye kwa sasa ni marehemu ikidaiwa kuwa alipoteza maisha kutokana na dawa hizo, pamoja na shida alizokuwa akizipata msanii Ray C, za kutafuta dawa hizo hata usiku wa manane.
Na vile vile Mbunge huyo ameitaka mamlaka mpya wa dawa za kulevya kuwachunguza watu 97 ambao majina yake yamekabidhiwa hivi karibuni na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na yeyote atakayethibitika kuhusika, achukuliwe hatua, huku akionesha imani kubwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo, Dkt Rogers William Sianga.

from Blogger http://ift.tt/2lO2QeN
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment