MWANAJESHI MBARONI KWA TUHUMA ZA DAWA ZA KULEVYA

Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ni miongoni mwa watu 400 waliotiwa mbaroni mkoani Tanga kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Pia, taarifa zaidi ya 500 zinazohusiana na dawa za kulevya zimetolewa katika vituo vya polisi mkoani humo kuanzia Januari mwaka jana mpaka kufikia Februari 8 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alisema katika vita ya dawa za kulevya, Jeshi la Polisi likiwa katika doria limemkamata askari wa JWTZ , Koplo Rashid Mohamed kwa tuhuma za kukutwa na bunda 23 za mirungi. Alisema askari huyo alikamatwa Februari 9 akiwa na pikipiki, na polisi wanaendelea kufanya upelelezi wa tukio hilo kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa dhidi yake.
Alisema pia kuwa jumla ya watu 413 wamekamatwa na kwamba taarifa zipatazo 536 zinazohusu dawa za kulevya zimetolewa katika vituo mbalimbali vya polisi.
Dawa za kulevya zilizokamatwa ni pamoja na bangi tani 1.2, mirungi tani 2.6, na kilo 1,208 za heroine na cocaine. Alisema watuhumiwa waliokutwa na bangi ni 236, mirungi 125, na dawa za heroine na cocaine ni 56.
Kamanda Wakulyamba alifafanua kuwa kesi za bangi zimefunguliwa 315, za mirungi 165 na heroine na cocaine kesi 56.
Alisema mkakati wa jeshi hilo wa kukabiliana na wimbi la dawa za kulevya ni kudhibiti matumizi holela ya bandari bubu zipatazo 40 zilizopo katika wilaya za Tanga, Pangani, Mkinga na Muheza.

from Blogger http://ift.tt/2liEwAK
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment