Wasomi na wachambuzi wa masuala ya siasa, sheria na uchumi, wameeleza kushangazwa na kauli ya Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutokuwa na taarifa kuwa tayari Sheria ya Dawa za Kulevya imeanza kutumika, huku wengine wakimpongeza kwa kurejea kwenye mstari na kujipanga upya na vita kubwa ya dawa hizo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wamemtaka Rais kuendelea kuwa imara katika mapambano ndani ya misingi ya sheria.
Mchambuzi wa masuala ya kisiasa na uchumi, Dkt. Albanie Marcosy katika maoni yake alimshauri
Rais kuwawajibisha walioshindwa kumpelekea mapendekezo ya uteuzi wa watendaji wa Mamlaka
ya Kukabiliana na Dawa za Kulevya.
“Hii ina maanisha ule upungufu tuliokuwa tukiupigia kelele kwenye hatua zilizokuwa zikichukuliwa
na RC wa Dar es Salaam, Paul Makonda ulijitokeza kwa kutenda mambo bila kujua. Msema kweli
mpenzi wa Mungu, naamini anapaswa kusamehewa.
“Chondechonde, fuata sheria kwenye hili, isiwe kikwazo kwako siku za mbele. Kuwa imara na haswa ujue vita hii si lelemama, kuwa imara…. fumba macho, usiangalie,” alisema Dk Marcosy.
Profesa wa Sheria Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Josephat Kanywanyi alipongeza hatua zilizochukuliwa katika mambo ambayo yalipigiwa kelele kwenye vita hiyo akisema yamefanyiwa
marekebisho jambo ambalo ni jema.
“Rais ni mtendaji mkuu, kama amegundua kuna jambo lilikuwa nje ya mstari hivyo ameona
muhimu kulirejesha ni jambo zuri. Katika vita hii takatifu, inatakiwa ushirikiano na kuzingatia
sheria katika utekelezaji,” alisema Profesa Kanywanyi.
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook alisema sheria hiyo ilipatikana kutokana na wabunge kutoa hoja binafsi kuhusu dawa ya kulevya. Aliwataja wabunge hao kuwa ni Ester Bulaya na Dkt. Faustine Ndugulile na kwamba baada ya hoja hiyo, Serikali ilipeleka muswada bungeni ambako ilitungwa Sheria ya Kupambana na Dawa za
Kulevya mwaka 2015.
“Serikali mpya ikaingia madarakani Novemba 2015 na Februari 2017 ndipo kamishna mkuu
akateuliwa baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia kamati husika na kuzungumza
bungeni.
“Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo, lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa
instruments (majukumu), hizo hutaja kila sheria kwa kila Waziri, ilikuwaje akasahau sheria hii
nyeti…?” alihoji Kabwe ambaye baadaye alithibitisha kuandika ujumbe huyo kwenye mtandao.
HT: MWANANCHI
from Blogger http://ift.tt/2kp45kt
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment