Taarifa kutoka nchini Korea Kusini zinaeleza kuwa, kaka yake Rais Korea Kaskazini Kim Jong-un ameuwa katika uwanja wa ndege nchini Malaysia.
Kim Jong-nam mwenye umri wa miaka 45 inasemakana kuwa alikuwa akiliwa njama za kuuawa katika uwanja wa ndege Kuala Lumpur nchini Malaysia.
Vyanzo vya kuaminika kutoka nchini Korea Kusini vimesema kuwa mwili wa Kim Jong-nam unafanyiwa uchunguzi ambao hufanywa kwa mtu baada ya kufariki katika njia inayotiliwa shaka ili iweze kufahamika ni nini kimemuua (post-mortem examination)’
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Kim Jong-nam ndiye mtoto mkubwa wa Rais wa zamani wa Korea Kaskazini Kim Jong-il.
Maafisa wa Polisi kutoka nchini Malaysia amethibitisha taarifa hizo ambapo wamesema kifo hicho kimetokea wakati akikimbizwa kwenda hospitali kutoka uwanja wa ndege.
Serikali ya Korea Kaskazini haijazungumzia tukio hili au kuthibitisha kama ni kweli ni ndugu wa kiongozi wa nchi hiy0. Taarifa zote kuhusu tukio hili zimetolewa na serikali ya Korea Kusini.
Kwa mujibu wa runinga ya Chosun, kutoka Korea Kusini imesema kuwa Kim aliwekewa sumu na wanawake wawili alipokuwa katika uwanja wa ndege wanaoaminika kuwa wanatokea Korea Kaskazini. Taarifa hizi hazijathibitishwa pengine popote.
from Blogger http://ift.tt/2liuqQl
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment