Wachumba wawili kutoka nchini Kenya ambao habari zao zilisambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii baada ya kufunga ndoa iliyogharimu USD 1 (TZS 2233) wamedhaminiwa na kufanya sherehe nyingine ya kifahari leo katika maadhimisho ya siku ya wapendanao.
Wilson na Ann Mutura ambao kwa mara ya kwanza hawakuweza kugharamia kununua nguo za harusi na sherehe sasa wamefunga ndoa nyingine iliyogharimu dola za kimarekani 35,000 (TZS milino 78.2).
Awali waliahirisha ndoa yao mara mbili mwaka 2016 kutokana na ukata wa fedha kabla ya kuamua kufunga mwezi uliopita kwa gharama ya kununua pete peke yake. Wachumba hao walikwenda kanisani wakiwa wamevalia nguo zao za kawaida na kuamua kufunga ndoa.
Picha zao za ndoa ya pili na ya kifahari zimechapishwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii huku watu wengi wakiwapongeza kwa upendo wao waliouonyesha.
Hapa chini ni picha zao za leo wakati wa sherehe;
from Blogger http://ift.tt/2koUzOk
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment