Imekua desturi ya Nay wa Mitego kuandika mistari ya utata kwenye baadhi ya ngoma zake,kitu ambacho kimejitokeza tena pia kwenye wimbo wake mpya, Muda Wetu.
Kwenye ngoma hiyo, Nay amedai kuwa kuna wasanii ambao wanabebwa kwa kupewa promo kubwa lakini promo ikikata wanabaki hawana lolote. Kwenye mahojiano na kipindi cha Supermega kupitia Kings Fm kinachoongozwa na Prince Ramalove, Nay ameweka wazi kuwa anafahamu wasanii hao na yupo tayari kuwaweka hadharani.
““Nafikiri hiyo tuwape kazi wananchi watuorodheshee ni msanii gani kwa kipindi hichi anaishi kwa upepo wa promotion na upepo ukikata tutaona reaction zake,” amesema Nay.
Amedai kuwa yeye baada ya kupata matokeo makubwa ya ngoma hiyo,ataweka wazi list ya wasanii ambao anaamini kwa asilimia zote kuwa wanabebwa na washkaji zao ambao wapo kwenye vyombo vya habari.
CHEKA KIDOGO NA HUYU JAMA ASIEJUA KUCHEZA KWAITO
from Blogger http://ift.tt/2m28G8z
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment