NDEGE YA KAMPUNI YA QATAR AIRWAYS YAWEKA REKODI YA SAFARI NDEFU ZAIDI KWA NDEGE ZA ABIRIA

Ndege aina ya Boeing 777 ilipaa kutoka uwanja wa ndege wa Doha, Qatar siku ya Jumapili na ikatua katika uwanja wa ndege wa Auckland nchini New Zealand Jumatatu baada ya safari ya kilomita 14,535. Ilifika tena Doha katika safari yake ya kurudi usiku wa Jumatatu. Safari hii inatakiwa kuchukua muda wa saa 17 na dakika 30.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Qatar Airways, Akbar Al Baker ambaye alisafiri ndani ya ndege hiyo ilipofanya safari yake hiyo ya kwanza ya kwenda Aukland, alisema kuwa kuanzisha safari hiyo ya kutoka Qatar kwenda Aukland ni “inaipa kampuni hiyo nafasi nzuri” katika mkakati wao wa kuhakikisha wanatoa huduma dunia nzima.
Kabla ya kuanza kwenda Aukland, safari hii ilikuwa ikitawaliwa na wapinzani wao wa Emirates ambao kwa sasa wameshushwa hadi namba mbili baada ya Qatar Airways.
Ni ndege moja tu inayoenda masafa marefu zaidi, ndege ya Air India ambayo inaenda safari ya umbali wa kilomita 15140.71 kutoka uwanja wa ndege wa Delhi nchini India kwenda uwanja wa San Francisco nchini Marekani— lakini huwa inafanya safari fupi zaidi wakati wa kurudi.

Kwa sasa safari hii inayofanywa na ndege ya kampuni ya Qatar ndio safari fupi zaidi kati ya Doha na Auckland.

Kampuni nyengine za ndege hivi karibuni zimeanza kuongeza safari za masafa marefu ili kuwarahisishia usumbufu wateja wao.

Si muda mrefu kutoka sasa wasafiri wataweza kufanya safari kutoka Australia kwenda nchi za Ulaya moja kwa moja baada ya shirika la ndege la Qantas kutangaza mwezi Disemba mwaka jana kuwa safari ya kwanza ya moja kwa moja kwa abiria wao inatarajiwa kuanza mwezi Machi mwaka huu.


from Blogger http://ift.tt/2kpdQLq
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment