Mchezaji wa mpira wa kikapu kutoka Tanzania Hasheem Thabeet, amesema neno kukataa tamaa halipo kwenye misamiati yake na kwamba kwa alipotoka hadi akafika kucheza NBA ni baraka tele.
Thabeet ambaye hachezi tena kwenye ligi ya NBA baada ya kiwango chake kushika, alikuwa akihojiwa na CNN Ufilipino na anatajiwa kwenda kucheza kwenye mashindano Dubai baada ya kualikwa na klabu ya kikapu ya Mighty Sports ya Ufilipino.
Amedai kuwa anapoangalia mazingira aliyopitia hadi kufikia kuchezea ligi kuu ya mchezo huo Marekani , anaamini ana uwezo wa kurudi tena juu. “Ntaendelea kuendelea sababu nimeona jinsi nilivyofika kwenye hatua hiyo najua bado kuna nafasi nyingi sababu mimi bado ni kijana, nafanya kazi kwa bidii, wachezaji wenzangu wote wananipenda, hivyo naamini bado nina nafasi ya kucheza tena,” amesema.
Staa huyo amedai kuwa alichojifunza kwenye mchezo wa kikapu ni kuwa imara muda wote na kujua kuwa kuna wakati wa kushangiliwa na kuna wakati wa kupondwa. Anadai kuwa akipata nafasi ya kurudi tena NBA mashabiki watarajie kumuona Hasheem wa tofauti na kwamba anajua Tanzania nzima inamuangalia.
Akiongea kwa kujiamini Thabeet mwenye miaka 29 sasa, amemtolea mfano Dwayne Wade mwenye miaka 35 na bado yupo kwenye timu ya wachezaji wote bora wa Marekani na kwamba hata yeye umri wake bado unamruhusu kurejea kwenye ligi hiyo.
Kwa upande wa kualikwa na Mighty Sports kwenda kushiriki kwenye mashindano ya Dubai, anasema ni heshima kubwa na dunia nzima itauona uwezo wake.
from Blogger http://ift.tt/2kBRVzP
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment