Mwenyekiti wa Kkabu ya Yanga, Yusuf Manji amemtaka nahodha wa klabu hiyo na uongozi mzima kuhakikisha kuwa wanapambana mwanzo mwisho na kuwa matatizo yake yasiwapotezee muda.
Manji alitoa maneno hayo juzi alipokuwa bado yupo Hospitali ya Taifa Muhimbili katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alipokuwa akipatiwa matibabu. Akiwa hospitalini hapo alipata ugeni wa viongozi wa Yanga walioambatana na nahodha wa klabu hiyo kwa ajili ya kumjulia hali.
Ugeni huo alikuwemo pia kiongozi na mwakilishi wa wachezaji ndani na nje ya uwanja, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na msaidizi wake Haruna Niyonzima ulifika hospitali hapo maratu baada ya kutua kutoka Comoro walikokwenda kucheza mchezo wa Klabu Bingwa Afrika na kufanikiwa kupata ushindi wa 5-1.
Manji aliwaambia kuwa matatizo yake yasiwahusu hata kidogo kwani wanachotakuwa kukifanya ni kuhakikisha wanapambana kila anayekuja mbele yao apigwe goli nyingi za kutosha. Aidha, Manji aliwapongeza kwa ushindi walioupata Comoro na kutakiwa kushikilia hapo hapo bila kuyumbishwa na chochote.
Manji alitoka jana hospitalini hapo alipokuwa wamelazwa baada ya kupata matatizo ghafla akiwa Kituo cha Polisi cha Kati, Dar es Salaam anaposhikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Chanzo: Mwanaspoti
from Blogger http://ift.tt/2lUAWKc
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment