DAR ES SALAAM: Kufuatia msala wa kutuhumiwa kujihusisha na utumiaji au biashara ya madawa ya kulevya unaosimamiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, sasa baadhi ya mastaa wanadaiwa kukauka kwenye viwanja vya starehe.
Chanzo makini ambacho ni mmoja wa mastaa, alifunguka kuwa tangu sakata la kutajwa majina lilipoanza hali ni mbaya kwa mastaa hasa wa kike kwani waliokuwa wakiwapa fedha za kufanya mbwembwe mjini wengi wanahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa tayari.
“Ukweli hali ni mbaya kwa sisi mastaa ndiyo maana unaona hata zile mbwembwe za mjini hazipo tena, wengi tunahofia kutajwa huku wengine wakiwa wametajwa au wadhamini wao.
“Wasanii wa kike ndiyo wenye hali mbaya zaidi kwani wale mapedeshee waliokuwa wakiwapa jeuri wamepunguza kuwapa fedha huku wengine wakiwa wameshatajwa majina hali ambayo inaendelea kuzua hofu zaidi,” kilisema chanzo hicho.
Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili ulibaini kuwa, ni kweli hali ni mbaya kwa mastaa na wengi wao wakiwa na hofu kubwa baada ya kuona wenzao au watu wao wa karibu, wametajwa kwani hata wakipigiwa simu zao za mikononi wana hofu kuzipokea au hata wanapofuatwa majumbani mwao husemekana wamesafiri.
Uchunguzi huo ulibaini kuwa, kwenye kumbi mbalimbali za starehe jijini Dar, hivi sasa pamekauka kwani wahudhuriaji ni wachache huku mastaa wakiwa hawaonekani kama ilivyokuwa zamani walipokuwa wakijirusha.
Siyo kwenye viwanja tu, lakini pia hata ngoma mpya zilizoachiwa hivi karibuni hazina msisimko kwenye kumbi hizo kama zamani, mfano ukiwa ni wimbo mpya wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake wa Mary You akimshirikisha mwanamuziki wa Marekani, Ne-Yo.
Pia siku kadhaa zilizopita wasanii wakali kwenye Bongo Fleva, Diamond, Ali Kiba na Navy Kenzo walipata tuzo zilizotolewa Kampala nchini Uganda zilizojulikana kwa jina la Hapipo Awards, lakini hazikuwa gumzo kama kipindi kingine zinavyokuwa na hii yote ni kutokana na sakata la madawa ya kulevya.
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii, nako kumepoa kwani ishu kubwa inayojadiliwa ni masuala ya madawa ya kulevya jinsi watu wanavyotajw a , wale mastaa wa liozoea kuposti picha na mambo yao mbalimbali kwa sasa wanaonekana kupoa, jambo ambalo ni tofauti na zamani.
Baadhi mastaa ambao kabla ya ishu ya madawa ya kulevya walikuwa hawakosi klabu lakini sasa hawaonekani ni pamoja na Gigy Money, Amber Lulu, Aunty Lulu, Isabela Mpanda, Shilole, Wema, Uwoya, Baby Madaha na wengine kibao. Akizungumzia ishu hiyo, Amber Lulu alisema:
“Naona maisha yako vilevile, sina wasiwasi kwani wale waliokuwa wanategemea wanaume waliotajwa ndo’ wenye shida.”
Naye Isabela Mpanda alifunguka:
“Ni kweli, hali inazidi kuwa ngumu japokuwa huwa sipendi kwenda klabu kwani mimi ni mwanamuziki na sipendi kuonekana sana ili nisizoeleke.”
Aunty Lulu yeye alisema: “Mimi nilishabadilika hata kabla ya ishu za madawa ya kulevya ila kwa wale waliokuwa wanategemea wanaume wa madawa ya kulevya ndiyo wana hali mbaya na lazima mwaka huu tuheshimiane.”
from Blogger http://ift.tt/2lUzHuE
via IFTTT
0 maoni:
Post a Comment