Wanasayans wametengeneza njia ya ‘kuongeza akili kwenye ubongo’

Wanasayansi wametengeneza njia ya kuongeza akili kwenye ubongo
Wanasayansi kutoka HRL Information and System Science Laboratory wametengeneza njia inayo fahamika kama Matrix-style kuongeza elimu/akili kwenye ubongo wa mwanadamu.
Wanasayans wametengeneza njia ya ‘kuongeza akili kwenye ubongo’
Hivi ushawahi kufikilia dunia ingekuwaje kama watu tusingekuwa tunahangaika kuelewa au kupata ujuzi wa darasani bila njia ya kusoma? Ingekuwaje kama elimu ya darasani ingekuwa inapakiwa vichwani mwa watu kama vile unavyohamisha nyimbo kutoka kwenye memory card moja kwenda nyingine fikiria mfano unataka kufahamu kuendesha gari halafu unaigiziwa tu huo ujuzi kichwani kwako pasipo kwenda VETA au chuo cha udereva.
Maisha yangekuwa rahisi sana. Katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia ya hali ya juu tunaona jinsi ma roboti wanavyo wekewa programu za kuwaendesha na kuwaongezea ujuzi. Sidhani kama kuna mtu ambaye hatotaka njia rahisi kama hii kwakweli!
Wanasayansi hao wamefanikiwa kutengeneza njia ambayo itatumika kupakia ujuzi au weledi kwenye ubongo wa mtu husika na njia hiyo haito gharimu kazi kubwa sana kufanikisha kwake wao wamesema ni njia rahisi mno ni sawa na kujitupa kitandani na kulala. Wanasayansi hao kutoka HRL Information and System Sciences Laboratory, katika jiji la California nchini Marekani wamekuwa wakifanyia utafiti teknolojia hiyo mpya na ya kipekee.
Dr.Philips ambaye ni kiongozi wa timu hiyo nzima ya hao wanasayansi waliofanikisha teknolojia hiyo anasema “Watu hawaamini nakusema kwamba ni miujiza lakini ni masuala ya kisayansi zaidi yaliyotumika kutengeneza mfumo huo, unapokuwa unajifunza kitu ubongo wako unabadilika kwa njia ya kitaalamu inayoitwa neuroplasticity”.
Pia alisema “Kwa kuwa tunaendelea na kuiboresha zaidi hii teknolojia tunategemea ianze kutumika kwenye vyuo vya udereva wa magari, mashuleni, vyuo vya ufundishaji wa lugha pamoja na sehemu zote elimu inapotolewa”.

from Blogger http://ift.tt/2l0Rumi
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment