Watangazaji wauawa wakiwa hewani

Waandishi wawili waliuawa wakati wakiwa hewani
Wanaume watatu wamekamatwa kufuatia mauaji ya watangazaji wawili wa kituo cha Radio waliokuwa hewani katika Jamuhuri ya Dominika.
Mmoja wa waandishi alikuwa akipeperusha matangazo kwenye ukurasa wa Facebook wakati alipopigwa risasi na kuuawa.
Kanda ya video imeonyesha matangazo hayo yakikatizwa ghafla na kisha mwanamke mmoja anasikika akilia “Risasi! Risasi! Risasi!”.
Polisi wamethibitisha shambulio hilo lilifanyika hapo Jumanne katika eneo la San Pedro de Macoris, mashariki mwa mji mkuu wa Santo Domingo.Haki miliki ya pichaEPAImage captionJamaa na Marafiki zimeanza kuomboleza kifo cha wawili hao
Waliouawa ni pamoja na mtangazaji Luis Manuel Medina na msimamizi wa matangazo Leo Martinez.
Mwanamke mmoja alijeruhiwa na anaendelea kupokea matibabu.
Simu za Nokia 3310 kurejea?
Wanaume waliokamatwa hawajafunguliwa mashtaka na polisi wanasema hawajui kilichosababisha mauaji hayo na kuongeza uchunguzi unaendelea.
Hapo mwezi Agosti mwaka 2015, waandishi habari wawili wa Marekani walipigwa risasi na kuuawa wakati wakitangaza kwenye runinga katika jimbo la Virginia.

from Blogger http://ift.tt/2liUT0m
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment