Waya wa Umeme Ulioungua Barabarani Kariakoo Wazua Taharuki

Waya ukiwaka moto katikati ya barabara, Kariakoo, Dar.
Zimamoto wakifanya juhudi za kuuzima moto huo. 
Polisi wakiwakamata waendesha bodaboda wasiokuwa na kofia ngumu.
Abiria waliokuwa kwenye mabasi ya mwendokasi wakishuka na kutimua mbio baada ya taharuki hiyo.
TAHARUKI kubwa imewakumba wafanyabaiashara na wa Kariakoo na wananchi wengine waliokuwa maeneo hayo baada ya kukatika kwa waya wa umeme na kuangukia barabarani huku ukiwaka moto.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa 5: 30 mchana wakati askari polisi walipokuwa wakikamata waendesha bodaboda wasiokuwa na kofia ngumu za kundeshea (helmet) maeneo ya Msimbazi Kariakoo jijini Dar es Salaam na kusababisha shughuli za usafiri na biashara kusimama kwa takribani dakika 40 huku abiria waliokuwa kwenye mabasi ya mwendokasi wakishuka na kukimbia kufuatia moto huo kutanda katikati ya barabara.
Wananchi walijaribu kuuzima moto huo lakini ilishindikana hadi walipofika Kikosi cha Zimamoto ambao waliumwagia mchanga ukapungua japo haukuzima, ndipo wakaamua kupiga simu makao makuu ya Shirika la Umeme Tanzania  (Tanesco) ambapo mafundi walifika na kuuzima.
Aidha kwa mujibu wa fundi wa umeme kutoka Tanesco, Shadrak Kapinga amesema kuwa, chanzo cha moto huo kilikuwa ni kutokana na waya kuchoka hivyo kukatika na kusababisgha moto kuwaka.
Zimamoto wakikaza kuuzima moto huo.
Nguzo ambapo waya huo ulikatika.
Moto baada ya kuzimwa.
Pichaz: Gabriel Ng’osha na Ibrahim Mussa/GPL

from Blogger http://ift.tt/2k535Ae
via IFTTT


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment