Picha: EFM yapewa ruksa ya kuruka mikoa 10 ya Tanzania, Nape amsifu Majay kwa uwekezaji mkubwa



Baada ya kufanya vizuri na kupata mashabiki wengi katika mji wa Dar es Salaam na Pwani, kituo cha redio cha EFM sasa kimepanua matangazo yake ambapo kinaanza kusikilizwa katika mikoa mingine tisa ya Tanzania.
Picha ya Majay wakwanza kushoto, akifuatiwa na waziri Nape, watatu ni mkurugenzi wa habari maelezo Hassan Abbas na mkurugenzi wa TCRA Francis Ntobi
Akiongea mbele ya mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kwa niaba ya mkurugenzi wa EFM na TVE, General Manager wa EFM, Dennis Ssebo amesema TCRA imeipa kipali kituo hicho kuanza kurusha matangazo yake kwenye mikoa tisa ya Tanzania.
“Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imeipa kibali EFM kwenda mikoani na tunaingia kwenye mikoa tisa. Hiyo ndio habari kubwa ambayo mkurugenzi wa EFM alitaka kuzungumza na wananchi hii leo ni kwamba tumepewa ridhaa ya kwenda kwenye mikoa tisa. Mikoa hiyo ni ifuatayo Mbeya, Tanga, Mwanza, Mtwara, Manyara, Singida, Kigoma Tabora na Kilimanjaro.”

Naye waziri Nape Akitoa hotuba yake amesema kuwa hakuwa anategemea kuona uwekezaji mkubwa uliofanywa na kituo hicho ambao ameuona na kutoa pongezi nyingi kwa bosi wa kituo hicho DJ Majay.

“Mnavyoonekana nje sivyo mlivyo ndani. Ndani kuna uwekezaji mkubwa wa teknolojia kubwa na hakika gharama iliyotumika kuwekeza hapa ni kubwa sana, sisi kama serikali tunakupongeza sana na tunakutakia kila la kheri. Na ninakuahidi serikali tutakupa ushirikiano na msaada unaouhitaji kuhakikisha uwekezaji huu unasonga mbele,” amesema Nape.
Wakati huo huo kituo cha EFM kimetengeneza mdundo (beat) la wimbo wa hamasa kwa wananchi ambao Diamond na Alikiba wanadaiwa kuwa wataingiza sauti zao kwa ajili ya kuipa nguvu timu ya Serengeti Boys ambayo imefanikiwa kufuzu kucheza michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana mwaka huu nchini Gabon.
Ntuli ambaye ni kiongozi wa upande wa production TVE akimuelekeza jambo mhe. Nape





Mkurugenzi wa EFM na TVE, Majay akiongea na mkurugenzi wa TCRA Ntobi na mkurugenzi wa habari maelezo Hassan Abbas
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment