Akizungumza na Gospo Media alisema kuwa,maandalizi yote yapo katika hatua za mwisho mwisho ili kulifanya tamasha hilo kuwa la kipekee na la namna yake.
‘‘Kiukweli maandalizi ya uzinduzi wa albamu yangu ya Kuna Namna yamekamilika kwa upande wa mazoezi na vyombo,ni kwa sehemu ndogo sana ambayo nayo nikishirikiana na watu wangu wa karibu tunaelekea kukamilisha ni kwa kumpata mgeni rasm wa siku hiyo pamoja na waimbaji watakao nisindikiza ama kunisapoti wakati wa uzinduzi wa albamu yangu pia nimesikia watu wameanza kuulizia nitafanyia wapi kwa maana ya ukumbi naomba kuwaambia watulie kwa sasa maana nimepata maeneo mengi, sasa ninachokifanya na kamati yangu ni kuchagua wapi tukafanyie uzinduzi na tukishapata mapema sana tutawataarifu wapenzi na wafuasi wa muziki wa injili ili waje siku hiyo tumsifu na kumtukuza Mungu”.Alisema Rogate Kalengo.
Mwimbaji huyo anayetamba kwa nyimbo zake mbili mpka sasa kama Kuna Namna pamoja na wimbo wake aliuachia juma moja lililopita uitwao Ombi Langu na ambao unafanya vyema mpaka sasa kwenye media mbalimbali hapa nchini.
Kwa mawasiliano na Rogate kalengo
facebook;Rogate Kalengo
Instagram;@rogate-kalengo
Whatsapp and calls;+255(0)752 254 801.
0 maoni:
Post a Comment