Meya wa jiji
la Mbeya David Mwashilindi amewataka Viongozi pamoja na wananchi kutoharibu
maendeleo kwa itikadi za kisiasa.
Hayo
ameyasema wakati akiweka jiwe la msingi la zahanati katika kata ya Tembela na
Mwasanga ambapo amesema kuwa wakati huu sio wa siasa bali ni wakati wa kufanya
maendeleo.
Awali
akisoma risala kwa mgeni rasmi afisa mtendaji wa kata ya Tembela Obel Yesaya
amesema kuwa ujenzi wa zahanati hiyo ni kwa ushirikiano wa kata mbili ambao
ulianza February mwaka 2016 na ujenzi
huo ni kwa nguvu ya wananchi ambao wamechangia jumla ya shilingi million 9.
Akijibu risala hiyo Mwashilindi amewataka viongozi kujikita katika
maendeleo ya ujenzi wa zahanatu pasipo kuangalia itikadi zao za vyama na
amechangia tani moja ya simenti ili kukamilisha ujenzi.
Naye
mwenyekiti wa wilaya Chadema Obadia Mwaipalu amesema kuwa ili ujenzi wa
zahanati uweze kukamilika unahitaji umoja na mshikamano.
Kwa upande
wao madiwani wa kata hizo mbili Diwani Joel Okoka (CCM) na Andason Ngao
(CHADEMA) wamesema kuwa wao ni vyama
tofauti lakini wamesema utofauti wa vyama hawawezi kuuingiza katika suala la
maendeleo.
Nao wananchi
wa maeneo hayo wameshukuru kwa kuweza kuanza ujenzi wa zahanati hiyo kutokana
na huduma hiyo kuwa mbali na wanawake wamekuwa wakipata shida wakati wa
kujifungua na wakati mwingine kujifungulia njiani.
0 maoni:
Post a Comment