MAHAKAMA YA TABORA IMEMHUKUMU KIFUNGO CHA MAISHA JELA KWA HATIA YA KUMNAJISI MJUKUU WAKE.



MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nzega mkoani Tabora imemhukumu kifungo cha maisha jela, mkazi wa kijiji cha Ng’onho, kata ya Migua, wilayani hapa, Lubasha Ngasa (62) baada ya kupatikana na hatia ya kumnajisi mjukuu wake mwenye umri wa miaka minne.
 

Akisoma hukumu hiyo hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Serafina Nsana alisema kutokana na ushahidi usioacha shaka uliotolewa mahakamani hapo, mahakama hiyo imeridhia kumhukumu Ngasa kifungo hicho cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia hiyo.

Awali, mwendesha mashitaka wa polisi wilayani Nzega, Melito Ukongoji aliiambia mahakama hiyo kuwa Ngasa alilitenda kosa hilo Aprili 24, mwaka 2016 saa 3 asubuhi katika kijiji cha Ng’onho baada ya mtoto huyo kuachwa na wazazi wake waliokwenda kulima na Ngasa kuutumia muda huo kumbaka mtoto huyo.

Ukongoji alidai kuwa baada ya muda wazazi wake walisikia kelele za mtoto na walipoenda walikuta tayari mzee huyo keshamharibu mtoto.

Aidha mwendesha mashitaka huyo aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa kwa kitendo hicho cha kinyama alichokifanya ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia na tabia kama hizo.

Ngasa alipopewa nafasi ya kujitetea, aliiomba mahakama impunguzie adhabu kutokana na kuwa na umri mkubwa na kuwa ni tegemeo kwa familia yake. Utetezi huo haukuridhiwa na hakimu alimhukumu kifungo hicho cha maisha jela.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment