Chama cha wachezaji soka wakulipwa Uingereza (PFA) kimetaja kikosi chake bora cha ligi hiyo kwa msimu huu unaoelekea ukingoni.
Timu ya Chelsea na Tottenham Hotspurs ndizo zimeongoza kutoa wachezaji wengi katika kikosi hicho ambapo kila timu imetoa wachezaji wanne. Wachezaji wa Chelsea walioingia katika kikosi hicho ni pamoja na Gary Cahil, David Luiz, N’golo Kante na Eden Hazard.
Nao waliochaguliwa kutoka Spurs ni Kyle Walker, Danny Rose, Dele Alli na Harry Kane. Wachezaji wengine walioingia katika kikosi hicho ni David De Gea (Manchester United), Sadio Mane (Liverpool) na Romelu Lukaku (Everton).
0 maoni:
Post a Comment