Kituo cha habari cha CBC News cha Canada kinasema kwamba katika wikendi ya Pasaka, barabara kuu ya Southern Shore karibu na mji wa Ferryland ilifungwa baada ya wapiga picha - wataalamu na watu wa kawaida - kufika kwa wingi kupiga picha jiwe hilo la barafu.
Mawe hayo mara nyingi huwa yamevunjika na kuwa vipande vya vidogo vya barafu na husalia kwenye bahari hadi mwishoni mwa majira ya kuchipua na mapema majira ya joto.
Lakini dalili zinaonesha jiwe hili kubwa limekwama na huenda lisihame, kwa mujibu wa meya wa eneo hilo Adrian Kavanagh.
Masiwa ya barafu mara nyingi huwa na sehemu yake kubwa chini ya maji na ni sehemu ndogo tu ya ncha yake ambayo huonekana juu ya maji.
Hii huifanya kuwa rahisi kwa masiwa hayo kukwama yanapokuwa karibu na ufukwe.
0 maoni:
Post a Comment