Siasa imevamiwa na ‘manungayembe’ – Nape Nnauye






Aliyekua waziri wa habari, sanaa na michezo, ambaye ni mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amesema kuwa siasa ni ushindani wa hoja sio nguvu, baada ya Jumamosi hii, Chama wa wananchi CUF, kuvamiwa na Watu wasiofahamika, wakiwa na bastola na kuvamia mkutano huo uliotakiwa ufanyike Mabibo jijini Dar es salaam .

Mheshimwa Nape ameonesha kusikitishwa na tukio hilo, huku akihoji ‘Tunaenda wapi kama watu wanachukulia siasa ni nguvu.’
“Siasa ni ushindani wa HOJA sio NGUVU! Tunaenda wapi huku jamani?! Wanavamia na kutoroka??!! How?!! Siasa imevamiwa na manungayembe sasa,” ameandika Nape kupitia ukurasa wake wa Tweeter.
Sambamba na kuweka ujumbe huo, aliambatanisha na picha ya tukio hilo lililotokea kwa wananchi wa CUF, picha hii:

Na Emmy Mwaipopo
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 maoni:

Post a Comment