Mwenyekiti wa Chama cha
Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe amefunguka na kusema kitendo
cha Tanzania kushindwa kutumia fursa ya kilimo cha umwagiliaji ni kitu
ambacho kinamuumiza na kusema hicho ni kitu kinachorudisha nyuma
maendeleo.
Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe
Rungwe
amesema yeye angekuwa Rais wa nchii angehakikisha Watanzania wanalima
mara nne kwa mwaka kwa kilimo cha kumwagilia na si kutegemea kilicho cha
mvua, na kusema Mungu ametujalia karibu kila kitu ila tunashindwa
kutumia rasimali hizo jambo ambalo linatia aibu.
"Mimi ningemwagilia kwa
kutumia ndege za kumwagilia maji mabuza yale ningemwagilia mashamba.
lile bonde la Shinyanga pale mimi naona aibu sana, mimi ningehakikisha
Watanzania wanafanya kazi wanalima kwa mwaka mara nne siyo lazima tulime
mashamba nchi nzima bali tungelima mashamba ambayo yangetupa hadhi,
nasema mimi ningefanikisha" alisema Rungwe
Rungwe alikwenda mbali zaidi na kusema suala la kuhamisha maji ni
jambo ambalo linawezekana na kutolea mfano nchi ambazo kiasili ni jangwa
lakini saizi wanafanya kilimo baada ya nchi hizi kuchukua udongo sehemu
nyingine na kupeleka kwao na kufanya kilimo.
"Kwani unafikiri huko nje
wenzetu wanafanyaje, hata ukieenda hapo Israeli au ukienda Saudi Arabia
nchi nzima imelimwa? Wale wanahamisha udongo kutoka nchi zenye udongo
mzuri wenye rutuba wanapeleka jangwani wanatengeneza mashamba na
wanapata matunda mazuri wanauza dunia nzima, sasa itakuwa sisi ambao
Mungu katujalia ametupa kila kitu bure tunashindwaje kuhamisha maji,
wakati Benki ya dunia ipo, IFM ipo na nchi ndiyo zamana" alisema Rungwe
0 maoni:
Post a Comment