Wataalam wa Marekani wanaochanganua picha za setlaiti kutoka
Korea Kaskazini wanasema kuwa wameona kitu kisichokuwa cha kawaida
katika kituo cha nuklia cha taifa hilo: Uwanja wa mpira wa wavu.
Haki miliki ya pichaDigitalglobe/Getty Images Image caption
Picha za setlaiti zinaonyesha kwamba mchezo wa mpira wa wavu unaendelea
Picha hizo
zilichukuliwa siku ya Jumapili na setlaiti moja ya kibiashara huku
kukiwa na uvumi kwamba Pyongyang ilikuwa inajiandaa kufanya jaribio la
sita la kombora la kinyuklia wakati ambapo kuna wasiwasi kati yake na
Marekani.
Picha hizo zilitolewa na 38 North, mradi wa kuchunguza wa Korea kaskazini katika chuo kikuu cha Johns Hopkins huko Maryland.
Wachanganuzi
hao walitoa sababu mbili kwa yaliokuwa yakitendeka katika kituo hicho
cha Punggye-ri: Huenda maandalizi yalikuwa yamesitishwa ama ni mpango wa
udanganyifu unaofanywa na serikali.
Hatahivyo walisema katika ripoti yao, kwamba kituo hicho cha
Punngye kiko tayari kuandaa jaribio la sita la nyuklia wakati wowote ule
wakati agizo litakapotolewa kutoka Pyongyang.
Hadhi ama uwezo wa kituo hicho haijulikani ,mtaalam Joseph S Bermudez Jr, Jack Liu na Frank Pabian walisema.
Maelezo
ya vitendo vya hivi karibuni yanasema kuwa kituo hicho na maandalizi
yake ya kufanyia majaribio kombora la sita la nuklia yamesitishwa kwa
muda huku wafanyikazi wakiruhusiwa kwenda mapumziko.
Pyongyang
imesitisha vitendo vyake katika kituo hicho kama mpango wake wa
kimkakati na kuchelewesha jaribio hilo la kombora la sita la kinyuklia
hadi wakati ambapo utibuzi wake utalipatia fursa ya kisiasa.
Haki miliki ya pichaDigitalglobe/Getty Images Image caption
Picha za setlaiti zinaonyesha kwamba mchezo wa mpira
wa wavu unaendelea katika kituo cha kinyuklia nchini Korea Kaskazini Picha hizo zinaonyesha uchimbaji uliokua ukiendelea
ambao huenda ukaonyesha kwamba kulikuwa na uchimbaji wa mahandaki
lakini hakujakuwa na utoaji wa maji katika mahandaki hayo yanayotumika
kufanyia jaribio kombora la kinyuklia.
Kumekuwa na uvumi kwamba
kiongozi wa taifa hilo Kim Jong un huenda akatoa agizo la kombora hilo
la kinyuklia ili kwenda sambamba na maadhimisho ya 105 ya kuzaliwa kwa
mwanzilishi wa taifa hilo Kim 11-sung Jumamosi iliopita.
Je ulimwengu utafanyaje?
Kumekuwa
na wasiwasi hivi karibuni huku Pyongyang ikionya Washington kutofanya
uchokozi katika jimbo hilo, ikisema iko tayari kulipiza kwa shambulio
la kinyuklia.
Marekani, kwa upande wake inasema kwamba wakati wa subira ya kimkakati dhidi ya Korea Kaskazini umekwisha.
Kituo hicho cha Pungye kiko katika eneo la milima kaskazini mashariki.
Korea
Kaskazini inasema kuwa imefanya majaribio matano ya kinyuklia mwaka
2006, 2009, 2013 na mwezi Januari pamoja na Septemba 2016.
Lakini swali ni je taifa hilo limepiga hatua gani katika mpango wake wa kinyuklia?.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 maoni:
Post a Comment